Newcastle wamezidisha nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Brazil Joao Pedro baada ya kujua kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 angependa kusaini katika kikosi cha Eddie Howe. (Telegraph)
Arsenal wamewasilisha ombi la kwanza la pauni milioni 46.8, pamoja na nyongeza ya pauni milioni 8.5, kwa Sporting kumnunua mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 27. (Record)
Bayer Leverkusen wako tayari kuwasilisha ombi la kumnunua kiungo mshambuliaji wa Manchester City, James McAtee, 22, dirisha la uhamisho litakapofunguliwa tena. (Sky Sports)
Napoli inashindana na vilabu kutoka Saudi Arabia kumsajili mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25, kutoka Liverpool. (Fabrizio Romano)
Fenerbahce ya Jose Mourinho ina nia ya kumsajili beki wa kulia Muingereza Kyle Walker, 35, kutoka Manchester City kufuatia kutofaulu kwake kwa mkopo AC Milan. (Times)
Everton wanavutiwa na kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Mbrazil Fred, 32, ambaye kwa sasa yuko Fenerbahce. (Sozcu)
Mshambuliaji wa Villarreal mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4 Mfaransa Thierno Barry, 22, pia analengwa na Everton msimu wa joto. (Times)
Aston Villa wameweka mikakati ya kumsajili winga Mhispania mwenye umri wa miaka 19 Jesus Rodriguez kutoka Real Betis. (Athletic)
Crystal Palace wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Millwall Muingereza Japhet Tanganga, 26, ambaye anasemekana kuwa na kifungu cha pauni milioni 1.2 cha kutolewa kwa vilabu vyote vya Ligi Kuu msimu huu. Sunderland, Leeds United na Burnley pia wana nia ya kumnasa. (Express)
Meneja mpya wa Tottenham Thomas Frank anapanga mpango wa kuwaleta winga wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25 Bryan Mbeumo na mshambuliaji wa DR Congo Yoane Wissa, 28, kwa Spurs kutoka klabu yake ya zamani ya Brentford. (Guardian)
Rangers wanatazamiwa kumwachia Cyriel Dessers mwenye umri wa miaka 30 kujiunga na AEK Athens, huku mshambuliaji huyo wa Nigeria akikubali mkataba wa pauni 30,000 kwa wiki na timu hiyo ya Ugiriki. (Daily Record)
Roma wameanza mazungumzo na Brighton kumsajili kiungo wa Denmark Matt O'Riley, 24. (Gazzetta)
Wolves wanavutiwa na kiungo wa kati wa Celta Vigo Mhispania Fer Lopez, 21. (Sky Sports, external)
Baada ya kumsajili Leroy Sane kwa uhamisho wa bila malipo, Galatasaray wamekutana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Manchester City Ilkay Gundogan, 34, ili kumpeleka Uturuki mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani. (Fanatik)
Manchester City wanatazamia kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Mahamadou Sangare, 18, kutoka PSG kwa mkataba wa miaka mitano. (RMC Sport )
Lazio wana nia ya kumsajili Ruben Loftus-Cheek, 29, kutoka AC Milan - na kumuunganisha tena kiungo huyo wa kati wa Uingereza na meneja wake wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri. (Daily Mail)
Marseille na Porto ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili winga wa Uswidi Roony Bardghji, 19, kutoka Copenhagen. (Fabrizio Romano)
0 Comments