Header Ads Widget

TAKUKURU YA BAINI UPIGAJI FEDHA ZA ADA KWA WANAFUNZI VYUO VIKUU.


Na Samwel Mpogole Mbeya.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya imeokoa kiasi cha zaidi ya millioni 17 fedha za wanafunzi 57 wa chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya MUST ambazo walizidisha kwenye malipo halali ya ada katika Akaunti ya chuo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Maghela Ndimbo inaeleza kwamba fedha hizo zililipwa na wanafunzi hao 57 wakiwa wanafunzi chuoni hapo, ambapo chuo hakikurejesha fedha kwa wanafunzi hao hadi walipo hitimu masomo yao.

Amesema baada ya kupokea malalamiko ya wanafunzi hao walifanya ufuatiliaji na baada ya kubaini hayo walichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuitisha vikao na uongozi wa chuo cha Must ili kulipa fedha za wanafunzi, ambapo hadi kufikia sasa  wanafunzi wote 57 wamelipwa madai yao.

Katika hatua nyingine taarifa  hiyo ya Maghela Ndimbo, imeeleza kufanikiwa kurekesha kiasi cha shilingi millioni 30 kwenye akaunti ya marejesho ya mkopo ya asilimia 10 kwa halmashauri ya wilaya ya Mbarali baada ya moja ya kikundi kupewa mkopo huo January mwaka huu na kutumia tofauti na malengo ya maombi yao.

Imeeleza kwamba fedha hizo zilitolewa kwa kikundi cha watu watano ambao waliomba  kwaajili ya kilimo cha mpunga lakini baada ya kupewa fedha hizo waligawan kwaajili ya matumizi yao ambapo mtendaji wa kata alichukua kiasi cha millioni 17,500,000. Wakati wanachama wengine wa tano wa kikundi hicho wakigawana 2,500,000.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI