Mkurugenzi mkuu PDPC DKT Emmanuel Mkilia
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Ili kuongeza imani na wawekezaji kwenye taasisi na kampuni Tume ya ulinzi wa taarifa binafsi (PDPC) imetoa mafunzo kwa taasisi za umma na binafsi juu ya umuhimu wa kulinda taarifa binafsi kama haki ya msingi ya kibinadamu.
Akifungua hafla ya kunguza madhara ya vihatarishi kwa kutumia ulinzi wa taarifa binafsi June 23,2025 mkoani Arusha mkurugenzi mkuu wa PDPC Dkt Emmanuel Mkilia alisema kuwa Dunia ya leo ya kidigitali inayobadilika kwa kasi taarifa binafsi ziko hatarini kutumiwa vibaya.
"Umuhimu wa kulinda taarifa binafsi unatokana na sheria ya ulinzi binafsi sura ya 44 ambayo imeweka misingi thabiti wa kuhakikisha haki ya faragha na ulinzi wa taarifa binasfi inalindwa kama haki ya msingi,"Alisema Dkt Mkilia.
Alieleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha kila taasisi inatambua viatarishi vyote ambavyo vingeweza kusababisha tasisi isifikie malengo yake ambapo kwa sasa kuna changamoto kubwa katika kulinda faragha za mtu aliyekusudiwa kupata huduma na taasisi mbalimbali zinazotekeleza majukumu yake.
"Kipindi hiki imekuwa ni changamoto zaidi kwasababu ya teknolojia kwakuwa inataarifa nyingi za watu, lakini tumekuwa tuna improve business process na kila tasisi inatumia teknonojia kama njia na silaha ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi ndo maana mafunzo yanalenga kuhakikisha tunatambua viatarishi," Alieleza.
"Kwenye mafunzo haya tutapata uelewa wa kutosha ni kwa jinsi gani taasisi zetu na mambo gani ya kuyaangalia ili kuhakikisha taarifa binafsi inaendelea kupewa umuhimu lakini pia kuhakikisha kila taasisi inakuwa na utaratibu mzuri wa kutambua maeneo ya hatari lakini kuwa na uwezo qa kutambua viashiria na kuchukua hatua stahiki,"Alieleza.
Kwa upande wake mkurugenzi wa usajili na uzingatiaji wa PDPC Eng Stephen Wangwe alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kupinguza madhara ya viatarishi ambapo wameyqfanya kwa kushirikiana na taasisi ya usimamizi wa viatarishi na tutatoa namna ambavyo sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi itahusianishwa na masula ya viatarishi.
"Taarifa za mtu zinaweza zikampelekea kupata hatari hasa katika hizi taasisi ambazo zinachukua taarifa zetu kwaajili ya kutuhudimia kwahiyo kwasababu hiyo tunazifundisha ni mambo gani ya msingi ya kuzingatia katika ulinzi wa taarifa hizo ili wawe wamewalinda watu ambao taarifa zao zimekusabywa na wao," Alifafanua.
"Tutawafundisha misingi nane ya ulinzi wa taarifa binafsi lakini pia masuala ya ridhaa kwa kuhakikisha wewe ambaye wanatumia taarifa zako umetoa ridhaa ikiwa nj pamoja na namna gani ya kusimamia viatarishi ambapo inabidi wavitambue viatarishi na viashiria vyake na kuweza kuvikwepa(risk avoidance) au kuvipunguza (risk mitigation) au kuhanisha(risk transfer) na kuzifanyia zile zisizo na madhara makubwa uhakiki (risk approval)," Alisema
Naye Lusajo Jimmy mshiriki wa mafunzo hayo alisema kuwa kama taasisi itakuwa na mfumo mzuri wa kutambua viatarishi itasaidia kuaminika na watumiaji pamoja na kuvutia wawekezaji.
0 Comments