Na Shomari Binda-Musoma
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF ) mkoa wa Mara imewakumbusha wachimbaji wa madini umuhimu wa kujiwekea akiba.
Ukumbusho wa umuhimu huo wa kujiwekea akiba umetolewa jana juni 5,2025 na afisa matekelezo wa mfuko huo Athanas Rukuba wakati akitoa mada kwenye siku ya 2 ya kongamano la maonyesho ya madini mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex.
Amesema mfuko huo umeanzisha Skimu ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii kwa Sekta isiyo Rasmi ambayo wachimbaji walioajiliwa na kujiajili na sekta nyingine wanaweza kujiwekea akiba.
Athanas amesema uwekaji wa akiba una umuhimu mkubwa katika maisha ya baadae na serikali kupelekea kutazama upande huo.
Amesema kwenye kazi kuna Ä·upata ajali na kuumia pamoja na kuzeeka na kushindwa kufanya kazi hivyo akiba uliyojiwekea inasaidia kuendeleza maisha.
Afisa huyo wa NSSF mkoa wa Mara amesema kuumia na kuzeeka kutokana na akiba uliyojiwekea itasaidia pia kusomesha watoto na maisha mengine kuendelea.
Amesema taratibu za kujiunga na Skimu hiyo pamoja kuanza kujiwekea akiba ni rahisi na mtu anaweza kujiwekea akiba kwa njia ya simu kupitia malipo ya serikali.
" Ndugu zangu wachimbaji wa madini na wadau wote wa sekta ya madini NSSF mkoa wa Mara imekuja na ukumbusho kuhusu umuhimu wa kujiwekea akiba.
" Kwenye maisha ya kuwa kazini kuna kuumia na kuchoka kufanya kazi hivyo akiba utakayojiwekea itakuja kukusaidia hapo baadae tunawakaribisha sana kujiunga na NSSF tuwe na furaha baada ya kazi"amesema.
Sehemu ya wachimbaji walioshiriki kongamano hilo wamesema wamepata ukumbusho mzuri na wapo tayari kuanza kujiwekea akiba.
Wamesema kiasi cha shilingi elfu 30 kwa mwezi au zaidi sio kikwazo kwao na wengine walikuwa hawajawahi kupata elimu hiyo na kuishukuru NSSF mkoa wa Mara kwa kuweza kuwafikia.
Maonyesho na kongamano la madini mkoa wa Mara yanafikia tamati leo jumi 6,2025 kwa wachimbaji na wadau wa madini kufanya matembezi ya kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoamua kusaidia sekta ya madini yakiongozwa Waziri wa Madini Antony Mavunde na mlezi wa wachimbaji mkoa wa Mara mkuu wa mkoa huo Kanali Evans Mtambi.
0 Comments