Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro NCAA imewapongeza wadau mbalimbali wa Utalii wanaounga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya kuhakikisha hifadhi za Taifa zinatangazwa ili kuweza kukuza sekta ya Utalii nchini.
Akizungumza wakati akipokea ujumbe wa mapadri kutoka parokia mbalimbali za jimbo katoliki Singida Kamishna Msaidizi mwandamizi anayesimamia huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kupokea wageni wengi wa ndani na nje ya nchi ambao wanafunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kutimiza Azam ya utangazaji Utalii nchini.
Aidha amesema hatua hiyo ni jitihada za Serikali na wadau wa sekta binafsi kutangaza vivutio vya utalii nchini zinaendelea ili kuzaa matunda ambapo uongozi wa NCAA unahakikisha kuwa wageni wote wanapata huduma bora na kufurahia shughuli za utalii wanapokuwa ndani ya hifadhi.
Kwa upande wake Kiongozi wa mapadri hao, Padri John Makabe ameeleza kuwa, ziara yao imelenga kuona maajabu wa Mungu aliyoyaumba katika hifadhi ya Ngorongoro, vivutio vya utalii kama wanyamapori, malikale na mandhari mbalimbali zilizopo ili kwa nafasi zao wahamasishe jamii umuhimu wa uhifadhi na kutunza mazingira kwa manufaa ya wanadamu wote.
Jumla ya Mapadri 11 kutoka parokia mbalimbali za jimbo katoliki Singida wamefanya ziara ya kutembelea vivutio vya vya utalii katika hifadhi ya Ngorongoro na kusisitiza uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kuendelea kuvutia wageni wengi.
0 Comments