Header Ads Widget

MBUNGE WA KARATU DANIEL AWHAK ATUHUMIWA KUINGIZA WAGENI KWENYE MASHAMBA YA WAKULIMA MANG'OLA


Na Mwandishi Wetu Karatu.

MBUNGE wa Jimbo la Karatu (CCM) Daniel Awhak Tlemai anadaiwa kushirikiana na wageni kutoka nchi jirani na kuvamia mashamba ya wakulima wadogo wadogo wa Kata ya Mang'ola wilaya ya Karatu na kulima kama wazawa kinyume cha sheria.

Mbunge huyo anadaiwa pia kupora eneo kubwa la ardhi katika vijiji mbalimbali vya jimbo lake hivyo kudidimiza maendeleo ya wananchi hao.

Wakizungumza  Juni 23 mwaka huu Jijini Dar es Salaam kwa sharti la kutotaja majina yao wakazi wa Mang'ola walisema hatua ya  mbunge huyo kushirikiana wahamiaji  haramu kutoka nchi za jirani(Kenya) ambao huingia bila kibali imesababisha idadi yao kuzidi.

"Wahamiaji hawa haramu wamekuwa wakiingia Mang'ola kutokana na uhusiano wao na mbunge huyu na kufikia hatua ya kumiliki na kuhodhi ardhi kinyume cha  sheria" alisema mtoa taarifa hiyo.

Aliiongeza kuwa hali hiyo imetokana na mbunge huyo kuwakumbatia wahamiaji hao ambao ameingia nao mkataba na kufanya biashara ya ubia.

Habari zinaeleza kuwa mbunge huyo anadaiwa kuwaingiza raia hao  wakati alipokuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM-NEC na mkulima na mfanyabiashara wa vitunguu na mkazi wa kijiji cha Mbuga Nyekundu.

Mbunge Tlemai ambaye ni mkulima wa vitunguu  anadaiwa kumiliki hekari 1000 za mashamba ya vitunguu yanayozunguka shule ya Sekondari Domel iliyopo Mang'ola wilaya ya Karatu.

Inaelezwa kwamba mashamba ya mbunge huyo yanayoizunguka Sekondari ya Domel yamekuwa yakisababisha adha kwa wanafunzi kutokana na kuathiriwa na dawa kali zinazopulizwa kwenye mazao hayo ambazo wanafunzi hulazimika kuzivuta kutokana na kuvuta hewa yake kila zinapopulizwa.

Mashamba mengine ya  mbunge huyo po katika vijiji vya Qangdesh, Endamagar, Barai na Matala.

Alipotafutwa kujibu tuhuma hizo mbunge huyo alisema anamiliki ardhi hiyo kihalali.

Pamoj na mambo mengine Mbunge huyo akbaye alizungumxa na mwandishi kwa njia ya simu alizikanusha tuhuma zinazoelekezwa kwake akisema.zina.lengo la kumchafua.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI