NA PAUL WILLIUM, VUNJO.
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Charles Stephen Kimei, ameipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025.
Shukrani hizi zinatolewa kufuatia kukamilika kwa jengo la Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kyomu, iliyopo Kata ya Kahe Mashariki, kwa gharama ya shilingi milioni 63.
Mradi huu ni ushahidi wa dhamira ya kweli ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha huduma za afya, hasa kwa akina mama na watoto, na pia ni matokeo ya usimamizi madhubuti wa viongozi wetu katika ngazi zote.
Dkt. Kimei amesisitiza kuwa maendeleo haya ni matokeo ya mshikamano wa viongozi na wananchi, pamoja na nia njema ya serikali ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya karibu na makazi yake.
"Tutaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa kila Kitongoji, kijiji na kata kinaguswa na miradi ya maendeleo. Tunamshukuru sana Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa huruma na kujali wananchi wake, hususani katika sekta ya afya," amesema Dkt. Kimei.
Mwisho..
0 Comments