Header Ads Widget

MAJALIWA AZITAKA HALMASHAURI KUTEKELEZA MAHITAJI YA WATU WENYE UALBINO

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatumia fedha zinazotolewa kwao na serikali kuwapatia mahitaji saidizi wanafunzi wenye ulemavu na wenye ualbino bure kutokana na fedha ambazo serikali imekuwa ikipeleka fedha hizo kwenye halmashauri kwa ajili ya suala hilo.

Majaliwa amesema hayo mkoani Kigoma jana katika maadhimisho ya siku ya kujenga uelewa kuhusu watu wenye ualbino  yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre Mjini Kigoma akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa serikali imekuwa ikipeleka fedha kwenye halmashauri kwa ajili ya jambo hilo ikiwemo upatikanaji wa mafuta ya ngozi, miwani. Kofia.fimbo nyeupe na viti mwendo ambapo ametoa maagizo kwa  wakuu wa mikoa nchini kote  kusimamia maelekezo ya serikali katika kusimamia haki na mahitaji ya watu wenye ulemavu na wenye ualbino ikiwemo kupata vifaa saidizi.


Katika maadhimisho hayo Waziri Mkuu Majaliwa amezindua mfumo wa ukusanyaji takwimu kwa watu wenye ualbino maarufu kama Albino Mobile App ambapo ametaka takwimu zinazokusanywa kupitia mfumo huo kuwa sehemu ya kuandaa mipango, sera, sheria na mahitaji kwa watu wenye ulemavu na wenye ualbino.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu, Ridhwani Kikwete alisema kuwa wizara yake imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za watu wenye ulemavu na wenye ualbino kwa kuhakikisha mahitaji yao muhimu yanatekelezwa kikamilifu.


Kikwete alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ulemavu, kusimamia haki zao na kuweka mipango ambayo inahakisha mahitaji ya wenye uelemavu na wenye ualbino yanatekelezwa kwenye sera,sheria na mipango mbalimbali ya serikali na kwamba Albino Mobile App itakuwa nyenzo kubwa katika kusimamia haki na mahitaji ya watu wenye ulemavu na wenye ualbino.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha wenye ualbino nchini (TAS),Godson Mollel alisema kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa karibu na watu wenye ualbino na walemavu katika kutekeleza haki na mahitaji yao lakini yapo mambo ambayo hayajatekelezwa na kuiomba serikali kuyaangalia kwa karibu ikiwemi masula ya ajira, matibabu, vifaa vya kuwasaidia ikiwemo mafuta,kofia, miwano na uchache wa walimu maalum na shule maalum za watu wenye ulemavu.


Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa maadhimisho yam waka huu yanawapa nafasi wao kama wakuu wa mikoa wasimamizi wa karibu wa masuala ya ulinzi na usalama na mipango ya maendeleo kutafakari changamoto zinazojitokeza kwa watu wenye ulemavu na wenye ualbino na kuweka  mipango ya maendeleo kwa watu wenye ulemavu.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI