Header Ads Widget

BENK YA AKIBA COMMERCIAL YASHIRIKIANA NA CHUO CHA TIA KUPANDA MITI 1,500

 

Na Matukio Daima Media

Benki ya Akiba Commercial Plc (ACB) kwa kushirikiana na Taasis ya Uhasibu Tanzania (TIA), imepanda  miti 1,500 katika kampasi ya TIA ya Kurasini ikiwa ni sehemu ya juhudi endelevu za  kulinda mazingira  chini ya mpango wake wa Uwajibikaji kwa chini ya mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).


Zoezi hilo limefanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Afisa Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Wezi Mwazani,ambapo amesema hii dhamira thabiti  kwa vitendo imani ya benki katika suala la kulinda mazingira ni jukumu la pamoja kati ya taasisi na wananchi.


"Tuko tayari kuendeleza mpango huu katika kampasi nyingine za TIA tutakapohitajika,”aliongeza, akisisitiza utayari wa ACB kuendelea kushiriki katika juhudi za kimazingira kote nchini.


Meneja Mwandamizi wa Huduma za Wateja Binafsi ACB Emmanuel Mseti alitoa shukrani za dhati kwa uongozi, Chuo hiko wafanyakazi,na wanafunzi wa TIA kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha  kuwezesha kufanikisha tukio hilo.


“Zoezi hili si la ishara tu bali ni hatua ya vitendo inayoonesha dhamira yetu ya kulinda mazingira  ACB tunaamini katika kuchukua hatua halisi kupanda miti hadi kutoa huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali na mazingira ni kipaumbele chetu,” amesema Mseti.


Hata hivyo alieleza kuwa huduma za kidigitali za benki hiyo ACB Mobile, Internet Banking na Akiba Wakala 

zinaongeza upatikanaji wa huduma kwa ufanisi huku zikisaidia kupunguza matumizi ya karatasi, kuunga mkono mfumo wa kibenki unaolinda mazingira.


Mseti pia alitaja ushiriki mpana wa benki hiyo katika kulinda mazingira, ukiwemo mradi wa kuendeleza na kupendezesha  Uliofanyika Bustani ya Mnara wa Uhuru, jijini  Dodoma, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji ikiwa ni mfano wa mshikamano wa kweli na jamii.


Kwa Benki ya Akiba Commercial, kujitoa kwa jamii si hiari bali ni wajibu. Kuanzia elimu, afya, ushirikishwaji wa kifedha hadi utunzaji wa mazingira—benki inaendelea kujenga mustakabali jumuishi na endelevu kwa Watanzania wote.


Aidha Aliwasisitiza na kuwatia moyo wanafunzi wa TIA kuenzi miti hiyo kwa kuitunza ili iwe urithi wa kizazi sasa  na  kijacho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI