Header Ads Widget

WIKI YA MAZIWA KITAIFA MOROGORO

 

Na Lilian Kasenene,Morogoro 

KATIKA kuelekea maadhimisho ya wiki ya maziwa kitaifa, watanzania wametakiwa kutumia Elimu inayotolewa na wataalaamu juu ya umuhimu wa unywaji wa maziwa ili kupata lishe bora.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima alieleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya 28 ya wiki ya maziwa yanayoadhimishwa kitaifa  mkoani Morogoro kuanzia Mei 27 hadi Juni mosi Mwaka huu katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha ndege maeneo ya Fire katika  manispaa ya Morogoro.

Kutokana na umuhimu wa maziwa alisema ni vyema kukawepo kwa sera ya umuhimu wa tasnia ya maziwa ambayo itawafanya wazalishaji wa maziwa kufuga kwa ufanisi ng'ombe wa maziwa ili kufikia malengo ya kukuza uchumi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema kwa sasa Tanzania inakadiriwa mtu mmoja amekuwa  akinywa lita 67 za maziwa kwa mwaka ukilinganisha na nchi nyingine kama Kenya ambapo unywaji ni lita 130 na Uganda lita 70.

"Huko Duniani watu wanakunywa maziwa lita 360,370,kwa  nchi zinazoongoza kwa unywaji maziwa,lakini Afirika pekee inazalisha asilimia tatu(3)tu ya maziwa yanayozalishwa duniani ukilinganisha na nchi ya India   ambaye ndie mzalishaji namba Moja yeye anachangia asilimia 25,hivyo Bodi ya maziwa lazima iangalie fursa ya uzalishaji iliyopo kwa wafugaji,"alisema.

Alieleza kuwa wiki ya maziwa itatumika kuwaelimisha wafugaji na watanzania juu ya ufugaji kibiashara ambao utamfanya kukua kiuchumi kwa kufuga ng'ombe wa kisasa wawe wa upandikizaji ama njia nyingine na wenye tija.

"Kuna fursa kubwa kwa wafugaji,na masoko yapo Afrika,hili jambo la kuongeza uzalishaji wa maziwa linkwenda sambamba na kuelimishana, ni lazima tuweke mikakati,"alisema 

Wakati ambao bado sekta hiyo ya maziwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uzalishaji mdogo na kiwango Cha chini Cha unywaji wa maziwa akashauri wafugaji kuwa na jukwaa Moja la kuwakutanisha ili kuambizana mambo yanayowakabili na namna ya kuyatatua.

Malima alisema katika wiki hiyo kutakuwa na ugawaji wa maziwa kwenye vituo vya watoto yatima, Hospitali, pamoja na Magereza.

Mwakilishi wa msajili wa Bodi ya maziwa ambaye ni afisa masoko wa Bodi hiyo Said Isike alizungumzia Maendeleo ya program ya unywaji maziwa mashuleni ambapo alisema program hiyo bado inatekelezwa nchini katika mikoa 45, ambapo kwa Morogoro zipo shule mbili za msingi za Mafiga na mchikichini kwa wanafunzi kupata maziwa kwa bei nafuu.

Akasema katika shule hizo, kuna shule 5 ambazo zimefungiwa mashine maalum za kuuzia maziwa ATM, na kwamba bado kuna changamoto ya upungufu wa maziwa na uhaba wa mashine hizo ingawa bado program hiyo ni endelevu.

Isike alisema lengo la program  hiyo ni kuwafanya wanafunzi kuwa na tabia ya kupenda kunywa maziwa Kila wakati.

Mteknolojia wa chakula katika Bodi hiyo Rajilan Hilali alisema katika ukanda wa kitropiki na joto lililopo uzalishaji wa maziwa bado ni changamoto,hivyo kutokana na hali hiyo katika ukanda huo akashauri ufugaji wa ng'ombe chotara ili kupata walau wastani wa lita 10 hadi 15 kwa siku.

"Kwa mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya ndo unaweza kupata maziwa lita 20 kutokana na ukanda wa hali ya hewa kuwa baridi,"alisema Hilali.

Maadhimisho hayo yatafanyika Mei 27 Hadi Juni 1,2025 katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege Manispaa ya Morogoro na yatakwenda sambamba na  shughuli mbalimbali yakilenga kuhamasisha matumizi na uzalishaji wa maziwa

Kauli mbili ni 'Maziwa Salama kwa Afya Bora na uchumi endelevu,'




mwisho 


Amfumania mkewe na mtoto wa kambo!

Jina langu ni Juma Ally, leo nitasimulia hadithi ambayo imetikisa familia yangu kwa kiasi kikubwa, suala hili limeacha watu midomo wazi hata majirani na wakazi wa eneo hili. 

Kwa muda mrefu nilikuwa nikimshuku mke wangu kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtoto wangu wa kambo ambaye nilimuoa akiwa naye maana alikuwa akiishi naye hivyo nikawachukua kwa pamoja hadi nyumbani kwangu. 

Mashaka yangu yalikuwa yasiyoweza kuvumilika lakini sikutaka kuparamia suala hilo kwa pupa bila kuwa na ushahidi wa kuthibitisha  ukweli wa suala hilo, hivyo nikaamua kutafuta usaidizi kutoka kwa Kiwanga Doctors. 

Niliamua kufika kwa Kiwanga Doctors nikiwa na nguo ya ndani ya mke wangu ili waganga hao wajadi waweze kufanya matambiko yao na kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo. 

Basi walifanya matambiko yao ambayo husababisha wenzi wanaodanganya kwa wenza kwa kutoka nje ya ndoa au kuwa na mpango wa kando kukwama wakati wa kufanya tendo lao haramu. 

Hii ilikuwa hatua kali, lakini nilitamani sana kujua kama mashaka yangu yalikuwa ni kweli, nashukuru siku tatu hazikupita nilipokea simu ambayo ilinifahamisha kuwa kuna jambo la dharura ambalo limetokea. 

Mke wangu na mtoto wa kambo walikuwa wamekwama pamoja katika nyumba ya kulala wageni huko Mwingi wakati wakifanya mapenzi kama ilivyokuwa tamaduni zao za siku nyingi. 

Hivyo dawa na uchawi wa Kiwanga Doctors ulikuwa umefanya kazi, ukweli ulijidhihirisha kwa njia ya kushangaza zaidi. Nilikimbilia eneo la tukio, akili yangu ikiwa na hisia mseto pamoja na hasira. 

Lakini pamoja na hayo yote, nilijua nilipaswa kutatua jambo hilo, hivyo niliwaita Kiwanga Doctors ambao waliniongoza juu ya hatua muhimu za kuwatenganisha wawili hao hadi kufanikiwa. 

Kupitia jambo hilo nimejifunza ni bora kubaini ukweli mchungu kuliko kuishi kwa mashaka kama ilivyokuwa kwangu pindi nilipohisi ukaribu usio wa kawaida kati ya mke wangu na mtoto wa kambo.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba  +255 763 926 750  au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI