Header Ads Widget

WAZAZI, FAMILIA WALAUMIWA KUKWAMISHA VITA DHIDI YA UKATILI

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WAZAZI na Familia mkoani Kigoma  zimelaumiwa kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuzuia vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia unaotokea  kwa wanawake na watoto jambo linalofanya vitendo hivyo kuendelea.

kutokana na hali hiyo wadau mbalimbali wakiwemo Hakimu wa mahakama za Hakimu mkazi mkoa Kigoma na wilaya, waendesha mashitaka, maafisa wa dawati la jinsia la jeshi la polisi, maafisa maendeleo ya jamii na maafisa ustawi wa jamii kutoka halmashauri za mkoa Kigoma na watetezi wa kupinga ukatili kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kigoma wamekutana kutathmini na kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo.

Afisa maendeleo ya jamii katika sekretariet ya mkoa Kigoma, Msafiri Nzunuri alisema hayo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Wadau wa kupinga ukatili kutoa halmashauri sita za mkoa Kigoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa serikali wa kupinga ukatili unaotekelezwa kwa pamoja baina ya serikali na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya  Wanawake (UN WOMEN) kupitia mpango wa pamoja Kigoma (KJP).


Kwa upande wake Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya Kakonko,Ambilike Kyamba  ambaye ni mmoja wa washiriki wa mkutano huo alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria kali za masuala ya ukatili na unyanyasaji kijinsia bado wazazi na walezi wamekuwa chanzo kikubwa cha kuharibu ushahidi na wakati mwingine kutoa ushahidi unaowatetea watuhumiwa.

Babu Pascal ni Mkurugenzi wa Shirika la maendeleo la vijana Kigoma (KIVIDEA) alisema mila na desturi za kumkandamiza mtoto wa kike zimekuwa na athari kubwa hadi sasa hivyo elimu inapaswa kuendelea kutolewa ili kubadili mtazamo hasi kwa wasichana na wanawake uliopo kwa jamii ambao ndiyo chanzo cha vitendo vya ukatili na familia kushindwa kuchukua hatua madhubuti za kupambana na hali hiyo.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI