Header Ads Widget

JILL BIDEN ATAKIWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUPUUZIA AFYA YA MUMEWE

Mke wa Joe Biden ambaye aliongoza Marekani, Jill Biden ametakiwa kufikishwa mahakamani, akituhumiwa kutojali afya ya mumewe mzee.

Pendekezo la kumpeleka Jill Biden kortini lilipendekezwa na Leo Terrell, ambaye anakuwa afisa wa kutekeleza sheria katika idara ya uangalizi ya serikali inayosimamiwa na Elon Musk (DOGE).

Leo Terrell alisema kunapaswa kuwa na uchunguzi unaolenga kufahamu iwapo Jill Biden hakumshinikiza mumewe kuwania kiti cha urais wa Marekani, akijua wazi kuwa alikuwa na saratani.

Usiku wa Jumapili, Mei 18, 2025, ilitangazwa kuwa Joe Biden alikuwa amegunduliwa na saratani ya kibofu.

Joe Biden, ambaye aliongoza Marekani kwa muhula mmoja, hakuweza kuwania muhula wa pili kwa sababu ya masuala ya afya ambayo yalizuia chama chake cha Democratic kumteua.

Nafasi yake ilichukuliwa na Kamala Harris wakati huo kuwania kiti cha urais wa Marekani, lakini akaishia kushindwa na Donald Trump.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI