Header Ads Widget

WANANCHI NSOHO KUNUFAIKA NA ZAHANATI YA KWANZA TANGU KUUMBWA KWA ULIMWENGU


Wananchi wa Kata ya Nsoho, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, wameelekea kupata afueni kubwa ya huduma za afya baada ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa zahanati ya kwanza katika kata hiyo tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Mradi huo unaogharimu shilingi milioni 80, fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri, umefikia asilimia 22 ya utekelezaji wake, huku ujenzi ukiwa umeanza rasmi tarehe 1 Aprili 2025.

Katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Afrey Nsomba, kamati ya siasa ya wilaya ilipongeza juhudi za viongozi wa kata na ushirikiano wa wananchi katika kuhakikisha ndoto ya huduma bora za afya inatimia.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Ally Abdallah Mfaume, msimamizi wa manunuzi kata ya Nsoho, alisema kiasi cha shilingi milioni 80 kilichopokelewa kwa ajili ya mradi huo, tayari milioni 42 zimetumika, huku fedha zilizobaki zikiwa bado kwenye akaunti kwa ajili ya hatua zinazofuata za ujenzi.


Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Nsoho Juma Samsoni, alisema mradi huo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo ya jirani ambao kwa miaka mingi walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Wananchi nao hawakusita kuonesha furaha yao, wakieleza matumaini makubwa waliyonayo na kuahidi kushirikiana kwa hali na mali hadi mradi utakapo kamilika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI