Header Ads Widget

WANANCHI KANDA KUSAIDIKA NA UJIO WA MADAKTARI BINGWA.

Kutokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma za magonjwa mbalimbali unaosababishwa na ukosefu wa fedha, madaktari bingwa wamewasili jijini Mbeya na kuanza kutoa huduma katika kanda ya nyanda za juu kusini ili kuwapunguzia adha wananchi huduma itakayofanyika kwa muda wa siku tano kuanzia Mei 05 mwaka huu jijini Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya Dr. Abdalah Mbaga ambaye ni Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, amesema lengo la Serikali ni kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wote ili kuboresha afya zao kwa maendeleo endelevu.

Amesema mpango huo ni mkakati thabiti wa Serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya afya kuona wananchi hasa wasio na uwezo wanafuatwa na madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali badala ya wananchi kutumia muda mrefu na gharama kubwa kutafuta huduma mbali hasa kwenda Hospitali ya Taifa Mhimbili Dar es Salaam.

Kwa upande wake Katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile, amewaasa wananchi hasa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya hususani magonjwa sugu kutumia fursa hiyo kujitokeza kwa ajili ya kupata matibabu.

Uhagile amesema mpango huo wa Serikali ni mzuri kwa viongozi na wataalam mbalimbali kutoka ofisini na kuwafikia wananchi wake akieleza kuwa pamoja na mengineyo lakini pia utapunguza kadhia ya magonjwa ya yanayoikabili jamii hasa mkoani Mbeya.

Huduma ya madaktari bingwa kutoka Serikalini inatarajiwa kutolewa na madaktari kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wakiwemo kutoka Hosptali ya Taifa  Mhimbili, Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wataalam wa afya ya akili Hospitali ya Benjamin Mkapa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ambapo huduma hiyo inatarajiwa kutolewa kwa wananchi wa maeneo mbalimbali wa mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini ambayo ni mkoa wa Katavi, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Njombe na Iringa.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI