Header Ads Widget

KIBATALA "POLISI WAONGEZE UBORA WA KAZI,MDUDE APATIKANE"

 


Wakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, Peter Kibatala, amekemea vikali tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa kada wa chama hicho, Mdude Nyagali, huku akilitaka Jeshi la Polisi nchini kuboresha viwango vyao vya kiintelijensia na utendaji kazi ili kuzuia matukio ya aina hiyo.

Akizungumza siku ya Jumamosi mkoani Dar es Salaam kwa niaba ya mawakili wanaomtetea Lissu katika kesi mbalimbali, Kibatala amesema hatua ya watu wanaodhaniwa kuwa na mamlaka kuchukua mtu bila kufuata taratibu za kisheria, inazua maswali kuhusu usalama wa raia na weledi wa vyombo vya dola.

"Namna ambayo Mdude amechukuliwa, katika taifa hili ambalo Jeshi la Polisi linajinasibu kuwa na intelejensia mbalimbali, halafu mtu anakwenda kuchukuliwa huku kukiwa na taarifa za awali kabisa kutoka Mbeya zikionya kuhusu tishio dhidi yake, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuzuia tukio hilo," amesema Kibatala.

Ameongeza kuwa video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazoonesha michirizi ya damu ndani ya nyumba ya Mdude zinaashiria matumizi ya nguvu kupita kiasi, hali inayotia wasiwasi kuhusu uzingatiaji wa haki za binadamu.

"Tumeona video ikionesha damu ambayo tunaamini ni ya Mdude Nyagali, basi apelekwe kwenye vyombo vya sheria na tutashughulika na mambo hayo yote kisheria. Wale waliohusika ni watu wa chini kabisa kifikra na kimaadili- very basement people," amesema.

Ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama "kuongeza ubora wa kazi zao- step up their game - na wasiegemee intelejensia kwa masuala ya kisiasa tu kama vile kesi za Lissu, bali waelekeze nguvu pia kwenye kuzuia mashambulizi dhidi ya raia kama Mdude au Padre Dkt. Charles Kitima wa TEC ambaye pia alishambuliwa hivi karibuni."

Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilitoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo, likikanusha kuhusika na kukamatwa kwa Mdude. Taarifa iliyotolewa Mei 2, 2025, ilieleza kuwa mke wa Mdude, Bi. Sije Mbugi Emmanuel, aliripoti kuwa waumewe alivamiwa na watu wasiojulikana saa 2:00 usiku, wakamjeruhi na kumchukua kusikojulikana.

"Jeshi la Polisi linapinga vikali taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinazodai kuwa askari polisi wamehusika. Tunaendelea na uchunguzi na iitihada za kumtafuta.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI