Header Ads Widget

WANANCHI 7,000 WA MITAA ZA MINDU NA MGAZA WAOMBA SERIKALI KUWAJENGEA DARAJA LA KUDUMU

Na Lilian Kasenene,Morogoro

Matukio DaimaApp 

WANANCHI 7,000 wa mitaa ya Mgaza na Lugala Kata ya Mindu Manispaa ya Morogoro wameiomba Serikali kuwajengea daraja la kudumu ili kiunganisha mitaa hiyo na maeneo mengine ya kudumu.

Walieleza hayo wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari, ambapo walisema daraja hilo la muda lilijengwa kienyeji kwa magogo zaidi ya miaka mitano iliyopita kuharibia na kitishia maisha ya watu na Mali zao na hata kushindwa kufikia huduma za msingi kwa urahisi

Balozi  wa mtaa Mgaza Idd Kisala alisema pamoja na kukejengewa shule alimuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwajengea barabara ili kupata mawasiliano ambayo inasaidia wanafunzi kuvuka kwenda shule.

"Juzi tumemuokoa bodaboda alizama kwenye korongo hii ni barabara kubwa ya kwenda mazimbu,watoto watashindwa kwenda shule, tunaomba mama yetu na Waziri wa ujenzi watusaidie,"alisema.

Elizabeth Jonathani, mjumbe,mtaa wa Mgaza alisema kwa siku kadhaa watoto wamekosa kwenda shule kutokana na daraja kubomoka kutokana na mvua kuonyesha, mawasiliano ya pande mbili yamekatika.

Alisema wao kama wananchi wamejichanga na kuweka mbao za kawaida na wamekuwa wakitegemea kupeleka biashara upande mwingine, akaomba Serikali kuwashika mkono.

Kipindi hiki cha msimu wa mvua wananchi wa Kata hizi walibainisha kuwa daraja wanalovukia Sasa linashindwa kuhimili mazingira na limezidi kuwa hatari kwao.

Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA)Wilaya ya Morogoro Mhandisi Mohamed Muwanda alizungumzia hatua wanazochukua kutibu changamoto hiyo ambapo alisema mpaka sasa wanafanya tathimini na kupata gharama halisi ya ujenzi wa daraja.

Alisema pia wameendelea na kuweka na kishindilia mchanga na udongo, kufanya usanifu na kujua wingi wa maji,kujua aina gani ya daraja litanyengwa kama la maqw ana zege au chuma.

"Milioni 15 zitatumika kuchonga barabara na kishindilia kujaza kifusi kwenye makorongo madogo,Lile daraja na korongo kubwa tunaendelea nalo na tathimini, kule wananchi ni wengi na kuna malazi na wengine wanaenda mashambani,"alisema mhandisi Muwanda.

Eneo hilo Lina wananchi zaidi 7000

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI