Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amesema Serikali inatambua na kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, ambacho hadi sasa kimefanikiwa kutoa ajira kwa watu zaidi ya 445 pamoja na kuwa na vijana wa kujitolea zaidi ya 300,000 nchini kote.
Akizungumza leo Mei 10, 2025, katika hafla ya maadhimisho ya miaka 63 ya chama hicho, iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Dkt. Biteko alisema:
“Mmetoa ajira kwa wafanyakazi zaidi ya 445 na mmekuwa na vijana wa kujitolea 300,000 nchini nzima. Hili limewasaidia Watanzania kuendeleza moyo wa uzalendo na huduma kwa wengine bila kutegemea malipo.”
Dkt. Biteko aliongeza kuwa Chama cha Msalaba Mwekundu kina matawi na matawi madogo zaidi ya 700 kote nchini, hali inayorahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na watu wengine wenye uhitaji.
Aidha, alieleza mchango wa chama hicho katika kipindi cha mafuriko ya Desemba 3, 2023, yaliyotokea Hanang, Katesh, ambapo walijenga nyumba 35 kati ya 101 zilizopangwa kujengwa na Serikali — sawa na asilimia 35 ya mahitaji yote.
Dkt. Biteko pia alisifu ushiriki wa chama hicho katika kampeni za ukusanyaji damu salama tangu mwaka 1949 hadi sasa, pamoja na ujenzi wa kituo cha ukusanyaji damu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu mwaka 2017. Alisema juhudi hizo zimeokoa maisha ya watu wengi na kuzuia ongezeko la wajane, wagane na watoto yatima.
“Wakati wa janga la UVIKO-19, mlijitokeza kwa moyo wa kujitolea na kuwahudumia wagonjwa, mkiwa miongoni mwa wachache waliothubutu kufanya hivyo. Mmeokoa maisha ya Watanzania wengi,” alisisitiza Dkt. Biteko.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, David Kihenzile, alisema mfumo wa huduma ya kwanza bado haujaimarika ipasavyo nchini, kwani mara nyingi wahusika wa awali kufika eneo la tukio hukosa maarifa ya kutoa huduma hiyo.
“Katika kila watu 10 wanaopata ajali, ni watu watatu tu hupata huduma ya kwanza. Karibu asilimia 70 ya vifo hutokea kwa sababu ya kukosekana kwa huduma hii muhimu,” alisema Kihenzile.
Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Bi. Lucia Pande, alieleza changamoto ya mwingiliano wa majukumu baina ya taasisi mbalimbali wakati wa utoaji wa huduma ya kwanza, hali inayopunguza ufanisi wa Red Cross.
“Tunaomba Serikali itambue tofauti ya majukumu. Wanaosimamia wasibebeshwe majukumu ya kutoa huduma moja kwa moja, bali waachie taasisi yetu kutekeleza wajibu huo kwa ufanisi,” alisema Lucia.
Aidha, aliomba Serikali kuongeza bajeti ya chama hicho, kwani imekuwa ikipungua kila mwaka, na pia kuliwezesha kutoa huduma kwa njia ya "Commercial First Aid" ili mikoa iweze kujitegemea na kubaki hai katika utekelezaji wa majukumu yake.
Huku mkuu wa kitengo cha mawasiliano Tanzania Red Cross Society Seki Kasuka amesema kuwa wanajivunia tunajivunia kufanya kazi za ubinadamu na kuwa sehemu ya kusaidia serikali na jamii katika kutatua changamoto mbalimbali.
Seki amesema kuwa maadhimisho ya miaka 63 ya chama cha msalaba mwekundu yaliyofanika katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha Jakaya kikwete jiji Dodoma.
ameeleza kuwa leo wametimiza miaka 63 tangu kuanzishwa kwa msalaba mwekundu nchini na wanajivunia kwa sababu hakuna sekta ambayo hawajaigusa kama Red Cross.
"Tunayo miradi ya majanga ya njaa ambayo huwa tunawawezesha waathirika wa njaa kwa kuwapa pesa za matumizi sambamba na vyakula vya lishe na kuwapa mafunzo nanma ya kukabiliana na hali ya ukame wakati majanga mama yanapotokea".
aliongeza kuwa katika sekta ya maji tunajivunia
0 Comments