Header Ads Widget

WALIMU WAJENGEWA UWEZO WA KUFUNDISHA KIINGEREZA

 

Na Matukio Daima Blog 

WALIMU wa shule za msingi katika Halimashauri  23 za mikoa ya Tabora,  Arusha, Iringa na Rukwa wameanza kupatiwa mafunzo kuhusu mbinu za kufundisha Kiingereza ili kuwezesha wanafunzi kujifunza vyema lugha hiyo.

Mafunzo hayo yalianza tarehe May 05, 2025 katika vituo mbalimbali vya halimashauri za mikoa tajwa. 

Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na  kampuni ya Jolly Futures ambayo makao makuu yake yako Uingereza


 Mafunzo haya yanawahusisha walimu wa darasa la kwanza, walimu wakuu na wasimamizi wa elimu wa halmashauri.

Katika kituo cha Shule ya Msingi Mapinduzi kilichopo Manispaa ya Iringa, May 20, 

2025 walimu wameendelea na mafunzo hayo ambapo wanajifunza mbinu mbalimbali za ufundishaji Kiingereza zenye kuwajengea ujuzi wa kutumia mbinu ya Jolly Phonics kukuza stadi za Kusoma na Kuandika kwa Kiingereza kwa wanafunzi wa ngazi husika.


Mtaribu wa mafunzo hayo katika mkoa wa Iringa kutoka TET, Stephen Mwashihava, ameeleza kuwa kutokana na mbinu mbalimbali wanazojifunza kwa vitendo na kutumia zana bora walimu hao watakuwa bora sana kufundisha Kiingereza katika madarasa husika baada ya mafunzo hayo.  

 “Mafunzo  haya ni mahsusi kwa shule zinazotumia Kiswahili kufundishia kwa kuwa katika mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2023, lugha ya Kiingereza inaanza kufundishwa kuanzia Darasa la Kwanza katika shule hizo tofauti na zamani ambapo Kiingereza kilikuwa kinaanza kufundishwa Darasa la Tatu. 

Hivyo, kupitia mbinu hii ya Jolly Phonics, tunawajengea walimu uwezo wa namna ya kuwafundisha wanafunzi kusoma na kuandika kwa kufanya shughuli mbalimbali zilizopo kwenye muhtasari wanaoutumia shuleni, ikiwemo namna ya kutamka sauti za herufi, kutambua sauti katika maneno, kuunganisha sauti ili kusoma neno na namna ya kuandika herufi kwa maneno ya Kiingereza kwa usahihi.”

Mwashihava ameeleza kuwa katika kituo hicho jumla ya walimu 52 wanashiriki mafunzo hayo huku idadi ya walshiriki katika  mikoa yote minne yanakofanyika mafunzo hayo ni 4,200 wakiwemo walimu 2,000 wanaofundisha Darasa la Kwanza, walimu wakuu 1,900 na viongozi 300 wanaosimamia na kufuatilia  utekelezaji  wa mitaala shuleni ambao ni wadhibiti ubora wa shule, maofisa elimu taaluma wa wilaya na maafisa elimu kata.



Miongoni mwa walimu walioshiriki mafunzo hayo ni Mwalimu Etenes Msimika kutoka shule ya msingi Mshikamano, ambaye amesema mafunzo hayo yamempa mwanga mkubwa wa namna bora ya kufundisha Kiingereza kwa watoto wadogo.

“Awali tulikuwa tunawafundisha watoto Kiingereza bila mbinu rafiki, lakini kupitia mbinu ya Jolly Phonics nitaweza kuwafundisha wanafunzi wangu vizuri ikiwemo kutumia sauti na picha, jambo ambalo litawasaidia kuelewa haraka,” amesema Msimika.

Naye Mwalimu David Mkoma wa shule ya msingi Ugele amesema maarifa aliyoyapata yataenda kubadilisha kabisa namna anavyofundisha Darasa la Kwanza.

Mpango huo unatarajiwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika somo la Kiingereza na kuondoa changamoto ya wanafunzi kufika ngazi za juu za elimu kutokuwa na uwezo wa kuandika wala kuzungumza lugha hiyo kwa ufasaha.

Mwishoooo...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI