Header Ads Widget

TMA YAPOKEA UGENI KUTOKA ZIMBABWE

 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepokea ugeni kutoka Idara ya Huduma za Hali ya Hewa ya Zimbabwe (MSD) uliowasili nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu huduma za hali ya hewa.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za MSD kuboresha huduma zao kwa kujifunza kutoka kwa TMA, taasisi iliyotambuliwa kwa mafanikio yake makubwa katika kuimarisha huduma za hali ya hewa nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.



Ugeni huo umeichagua TMA kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya huduma za hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa, ushirikiano wa kikanda na kimataifa, pamoja na utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati kwa umma na wadau mbalimbali.

TMA imefurahishwa na ziara hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine barani Afrika kwa lengo la kuboresha huduma za hali ya hewa na kukabiliana na changamoto za mabadiliko

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI