Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima APP Dodo– Dodoma
WAZIRI wa Kilimo,Hussein Bashe, ameomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya Shilingi trilioni 1.24 kwa ajili ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Akiwasilisha makadirio hayo bungeni leo Mei 21, 2025, Waziri Bashe alisema fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo, matumizi ya kawaida na kuimarisha sekta za umwagiliaji na ushirika.
Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 838.2 zinahitajika kwa shughuli za wizara kuu, bilioni 382.1 kwa Tume ya Umwagiliaji, na bilioni 22.5 kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika.
Aidha, Wizara inatarajia kukusanya Shilingi bilioni 12.2 kutoka kwenye ada, tozo za ukaguzi wa mazao, umwagiliaji na ukodishaji wa mitambo.
Mwisho
0 Comments