NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
UJENZI wa Mradi wa Maji unaohudumia Kata za Okaoni, Kibosho Kati na Kibosho Kirima katika Tarafa ya Kibosho wilayani Moshi umekamilika kwa Asilimia mia moja.
Mradi huo wenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 500 ulifadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya Mradi huu kukamilika, hakuna tena kero ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Kata hizi.
Wakionyesha furaha yao, wananchi wa kata ya Kibosho kati wamedai kuwa kukamilika kwa mradi huo kumewasaidia kupata maji ya uhakika na salama muda wote.
Mariamu Faraja alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali, Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi, Diwani wa kata ya Kibosho kirima Inyasi Mushi, Diwani wa Kibosho kati, Bahati Massawe na Diwani wa Kibosho Okaoni, Morris Makoi kwa jinsi wanavyopambana kuwapelekea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwisho..
0 Comments