Header Ads Widget

TIMU YA RAS MARA BIASHARA UNITED VETERAN ZATOSHANA NGUVU UWANJA WA KARUME


Na Shomari Binda-Musoma 

TIMU ya Biashara United Veteran na RAS Mara zimetoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Karume.

Kocha mpya wa Biashara Veteran aliyechukua mikoba ya kuinoa timu hiyo Frumence Tungaraza amesema huo ni mchezo wake wa kwanza wa kiushindani tangu kuanza kuifunddisha timu hiyo na matokeo hayo sio mabaya kwake.

Amesema anaendelea kuona makosa ya timu hiyo anapopata michezo mbalimbali na lengo lake ni kuondoa jinamizi la kufungwa kwa timu hiyo.

Frumence ambaye aliwahi kuzichezea timu mbalimbali kwenye ligi ikiwemo Polisi Mara na Biashara United amesema timu anayoifundisha ina wachezaji wazuri ambao wanahitaji maelekezo kidogo ili wafanye vizuri.

Amesema ataendelea kuiandaa timu hiyo ili yatakapokuja mashindano mbalimbali waweze kufanya vizuri.

" Nashukuru mchezo umemalizika salama na naendelea kuiandaa timu yangu kwaajili ya mashindano mbalimbali.


" Yapo makosa ambayo nimeyaona na ntaenda kuyafanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi",amesema.

Kwa upande wake kocha wa timu ya RAS Mara Omary Hamis amesema timu yake imekuwa na mwendelezo mzuri katika kujiandaa na mashindano mbalimbali.

Amesema yapo mashindano ambayo yanakuja mbele yao na anaendelea kuiandaa timu ili itakapokwenda kwenye mashindano iweze kufanya vizuri.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI