Header Ads Widget

TANROADS IMEKAMILISHA UJENZI WA KM 109.49 ZA LAMI NCHINI, UJENZI WA KM 275.51 UNAENDELEA-WAZIRI ULEGA

BUNGENI DODOMA

SERIKALI imekamilisha Ujenzi kilomita 109.49 za barabara nchini kwa kiwango cha lami huku ikiendelea na ujenzi wa Kilomita  275.51, hali kadhalika ujenzi wa madaraja matano (5) unaendelea na ujenzi wa madaraja mengine matano (5) upo katika hatua za maandalizi.

Jumla ya kilometa 98.89 za barabara za mikoa zimejengwa kwa kiwango cha lami na jumla ya kilometa 192.89 zilikarabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Aidha, ujenzi/ukarabati wa madaraja madogo 12 kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na 13 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Waziri wa ujenzi Mhe Abdallah Ulega ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 5 Mei 2025 wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya ujenzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 bungeji Jijini Dodoma.

Waziri Ulega amesema kuwa miradi  saba (7)  ya barabara iliyokuwa itekelezwe kwa utaratibu wa EPC +F sasa inatekelezwa kwa utaratibu wa ‘sanifu na jenga’  (Design and Build). Hadi sasa,  maboresho ya kimkataba (addendum) ya miradi sita (6) yameshasainiwa. Aidha, mradi mmoja wa Igawa – Songwe – Tunduma sasa utatekelezwa kwa njia ya PPP, ambapo taratibu za kusaini mkataba zinaendelea. Sambamba na hilo.

Ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mkoani Tanga aliagiza ujenzi wa barabara ambayo hapo awali ilikuwa itekelezwe kwa utaratibu wa  EPC+F kutoka Kiberashi hadi Singida sasa utekelezwe kwa utaratibu wa  PPP. Tayari TANROADS na TPA wameanza majadiliano ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo hilo. 


Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 37,435.04. Kati ya hizo, kilometa 12,527.44 ni barabara kuu na kilometa 24,907 ni barabara za mikoa.

Katika mwaka wa fedha 2024/25, miradi ya barabara kuu iliyopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 385 kwa kiwango cha lami, ukarabati wa kilometa 35 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa madaraja 17, ukarabati wa daraja moja (1), kufanya maandalizi ya ujenzi wa madaraja tisa (9) na kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa madaraja mawili (2).

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI