Header Ads Widget

TRUMP ASEMA FILAMU ZISIZO ZA MAREKANI KUTOZWA USHURU WA 100%

 


Rais wa Marekani Donald Trump anasema atazitoza sinema zinazotengenezwa katika mataifa ya kigeni kwa ushuru wa 100%, huku akizidisha mizozo ya kibiashara na mataifa kote ulimwenguni.

Trump alisema alikuwa akitoa mamlaka kwa Wizara ya Biashara ya Marekani kuanza mchakato wa kutoza ushuru huo kwa sababu tasnia ya sinema ya Marekani inakufa "kifo cha haraka sana".

Alilaumu "juhudi za pamoja" za nchi nyingine ambazo hutoa motisha ili kuvutia watengenezaji wa filamu na studio, ambayo alielezea kama "tishio la Usalama wa Kitaifa".

Waziri wa Biashara wa Marekani Howard Lutnick alijibu tangazo la hivi punde, akisema "Tunaendelea". Lakini maelezo ya hatua hiyo hayako wazi.

Taarifa ya Trump haikusema iwapo ushuru huo utatumika kwa kampuni za uzalishaji za filamu za Kimarekani zinazozalisha filamu nje ya nchi.

Filamu kadhaa hivi karibuni zilizotolewa na studio za Marekani zilitengenezwa nje ya Marekani, zikiwemo Deadpool & Wolverine, Wicked na Gladiator II.

Haikuwa wazi pia ikiwa ushuru utatumika kwa filamu kwenye huduma za utiririshaji, kama vile Netflix, na zile zinazooneshwa kwenye sinema, au jinsi zitakavyohesabiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI