Header Ads Widget

TAKUKURU YATOA WITO WA USHIRIKIANO KWA WANANCHI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 

Wananchi wametakiwa kushirikiana kikamilifu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, ili kusaidia kupambana na vitendo vya rushwa na ukatili vinavyoweza kujitokeza.

Wito huo umetolewa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Maghela Ndimbo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Kamanda Ndimbo amesema ushirikiano wa wananchi ni muhimu ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki, amani na uwazi.


“Kuelekea uchaguzi, kuna viashiria vya baadhi ya watu kujaribu kutumia rushwa au vitendo vya ukatili ili kupata uongozi. Hili hatutalivumilia, tunahitaji wananchi kutoa taarifa kwa wakati,” amesema Ndimbo.

Katika hatua nyingine, Kamanda Ndimbo amesema TAKUKURU inaendelea kuchunguza tuhuma za rushwa ndani ya chama cha akiba na mikopo cha Mwanjelwa (Mwanjelwa SACOS). Ameeleza kuwa uchunguzi umefikia hatua za mwisho na watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika.

Amesisitiza kuwa taasisi hiyo itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa, bila kujali nafasi au hadhi yao katika jamii.

“Rushwa ni adui wa haki na maendeleo. Hatutasita kuwafikisha mahakamani wote watakaobainika kuhusika,” aliongeza.

TAKUKURU imesisitiza kuwa milango yake iko wazi kwa mwananchi yeyote mwenye taarifa za vitendo vya rushwa au matumizi mabaya ya madaraka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI