Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Uyole katika uchaguzi ujao.
Dkt. Tulia ametoa tamko hilo alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu Maalum wa Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo amsema kuwa ameamua kufanya uamuzi huo ili kuwahudumia wananchi wa Uyole kutokana na kasi ndogo ya maendeleo katika eneo hilo.
“Maendeleo ya Uyole yanasonga kwa taratibu sana. Nimeona ni vyema nijitoe kwa moyo wote kuhakikisha wananchi wa Uyole wanapata huduma stahiki na maendeleo ya haraka,” amesema Dkt. Tulia.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa licha ya kuhamishia nguvu zake Uyole, ataendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi kupitia taasisi yake ya Tulia Trust, ambayo inafanya kazi katika majimbo yote mawili na maeneo mengine.
0 Comments