Header Ads Widget

TAKUKURU MKOA WA KAGERA YAWATAHADHARISHA WATIA NIA UCHAGUZI MKUU.

 

Na Shemsa Mussa -Matukio daima                                  Kagera

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoani Kagera imesema haitasita kuwafuatilia na kuwachukulia hatua za kisheri watia nia wote kwa nafasi ya udiwani na ubunge watakwenda kinyume na taratibu na sheria zilizowekwa na serikali katika kupata uongozi.

Kauli hiyo imetolewa Hajinas Onesphory kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera  na wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika kipindi cha Januari hadi Machi 2025 kwa upande wa ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Onesphory amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu tayari Takukuru imeanza kufuatilia watia nia wote ambapo kila siku taasisi hiyo imejiwekea utaratibu wa kuhakikisha  inapata taarifa na kufuatilia.

Amesema kuwa watia nia hao wanaofuatiliwa ni wa nafasi ya udiwani na ubunge na kuwa taasisi hiyo ipo imara hivyo itachukua hatua kwa mtia nia yoyote atakayejaribu kukiuka taratibu zilizowekwa na serikali katika kupata uongozi.

"Sisi kama Takukuru tutaangaika na mtia nia atakayekwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali katika kupata uongozi"Onesphory.

Aidha kiongozi huyo amesema kuwa kwa mtu ambaye si mbunge hatoruhusiwa kujihusisha na matukio yakiwemo ya kiharakati ikiwemo michango, kuanzisha ligi za mpira , kutoa misaada kwa watoto yatima pamoja na matukio mengine mengi ya kijamii.


Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya taasisi hiyo ni kuzuia Rushwa ni jukumu lako na langu; tutimize wajibu wetu."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI