Header Ads Widget

SERIKALI,NYIHITA SUNFLOWER WAJA NA UFUNDISHAJI KILIMO BIASHARA RORYA

Na Shomari Binda-Rorya

SERIKALI kwa kushirikiana na kampuni ya Nyihita Sunflower wamekuja na utoaji elimu kuhusu kilimo biashara kwa wanafunzi na wananchi wilayani Rorya.

Elimu hiyo ni kuwafanya wakulima kulima kilimo cha uhakika na kuwawezesha kunufaika kiuchumi na kuweza kusaidia familia ikiwa ni pamoja na masuala ya elimu.

Akizungumza na wazazi na wanafunzi kwenye shule ya sekondari Mika iliyopo Wilaya ya Rorya jana mei 19,2025 baada ya kutoa elimu ya upandaji kwa wanafunzi,mkurugenzi wa kampuni ya Nyihita Sunflower Wilfred Nyihita amesema wazazi wasichukulie elimu hiyo kwa wanafunzi kama adhabu.

Amesema serikali na kampuni yake imekuja na mpango wa kuwainua wananchi kiuchumi kupitia kilimo na kama wanafunzi watashika elimu hiyo na kuwafikishia wazazi namna ya kupanda mbegu mashambani kila familia itainuka kiuchumi.

Nyihita amesema kilimo kwa sasa kimekuwa mkombozi na serikali kupitia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ipo began kwa bega na wakulima hivyo Rorya lazima iendane na fursa kilimo kupitia kilimo biashara.

Amesema lipo zao la alizeti ambalo haliliwi na ndege,ufuta,dengu,mbaazi,ufuta maharagwe pamoja mahindi ambayo ni mazao ya kibiashara na yamekuwa mkombozi.

" Naomba mniangalie vizuri namna bora ya kupanda mbegu kwa kutumia vipimo vya rula sentimita 15 kutoka shina moja kwenda lingine mstari kwa mstari.

"Elimu hii mnayoipata mwende muwafikishie wazazi nyumbani ili wanapokwenda shambani wapande kitaalamu na kupata mazao mengi na ya uhakika tumeelewana",amesema Nyihita alipokuwa akiwaelekeza wanafunzi wa shule ya sekondari Mika.

Nyihita amewaambia wanafunzi wa shule tatu za Mika shule ya msingi na sekondari pamoja na shule ya msingi Bukwe kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa kuwafikishia ujumbe wazazi kile walichojifunza.

Kwa upande wake Afisa Kilimo,Mifugo na Uvuvi wa Wilaya ya Rorya Gerende amesema kama mkuu wa idara anakwenda kupanga timu itakayoshirikiana na kampuni ya Nyihita kufanikisha jambo hilo.

Amesema wazo la Nyihita kuwainua wananchi kiuchumi kupitia kilimo biashara linepokelewa na serikali na wanakwenda kushirikiana kuhakikisha wanazifikia shule zote na kwa wananchi kupata elimu ya kilimo chenye tija.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI