Na Matukio Daima App.
ARUSHA.Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha kupitia kwa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Justine Masejo limetoa taarifa kwa kipindi cha kuanzia mwezi April mwaka huu hadi hivi sasa limefanya operesheni mbalimbali ambazo zimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 148 waliokutwa na makosa ya ubakaji, ulawiti, dawa za kulevya na pombe ya moshi.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa tarehe 20/05/2025 imeeleza yakuwa kwa upande wa makosa ya unyanyasaji wa kijinsia Jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa 51 ambao kati yao 29 walikutwa na tuhuma za makosa ya ubakaji na wengine 22 walikutwa na tuhuma za makosa ya ulawiti na mtuhumiwa 01 alihukumiwa kwenda jela kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za ubakaji na Watuhumiwa wengine kesi zao zipo katika hatua mbalimbali Mahakamani.
Kwa upande wa dawa za kulevya Jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 67 ambapo kati yao Watuhumiwa 29 walikamatwa wakiwa na Mirungi Kilogramu 969 na Watuhumiwa 22 wakiwa na bangi kilogramu 22.3.
Vilevile taarifa hiyo imebanisha kuwa watuhumiwa hao wa Dawa za kuelvya tayari walifikishwa Mahakamani ambapo Watuhumiwa 04 walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, mtuhumiwa 01 kifungo cha miaka 20 na wengine kesi zao bado zinasikisilzwa.
Pia jeshi hilo katika operesheni hizo limefanikwa kuwa kamata watuhumiwa 30 wakiwa na pombe ya moshi lita 210 na mitambo 9 ya kutengenezea kinywaji hicho haramu ambapo watuhumiwa wote tayari wameshafikishwa Mahakamani kwa taratibu za kisheria.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoani humo limewataka baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kuacha mara moja vitendo hivyo kwani litawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.
0 Comments