Header Ads Widget

SERIKALI YATANGAZA BEI YA PAMBA HUKU IKITOA MAELEKEZO.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi (mwenye tai) akishuhudia zoezi la Uzinduzi wa Ununuzi wa zao la Pamba katika msimu wa Kilimo 2025/2026.


Na Costantine Mathias, Simiyu.


SERIKALI kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba nchini (TCB), Wakulima na wadau wengine wa Pamba imetangaza Bei elekezi ya kununua zao la Pamba katika msimu wa kilimo 2025/2026, huku maelekezo mahususi yakitolewa kwa wakulima na Wanunuzi wa Pamba.


Akitangaza bei elekezi kwenye uzinduzi uliofanyika Mtaa wa Mwakibuga, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo Kenan Kihongosi amesema katika msimu 2025/2026, Pamba itaanza kununuliwa kwa shilingi 1,150/= kwa kilo moja daraja la kwanza na shilingi 575/= daraja la pili (Pamba fifi) na kwamba bei hiyo itaendelea kubadilika kadri ya soko la dunia.


Kihongosi amesema serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan imeweka utaratibu na jitihada za Jenga Kesho Bora (BBT) ambayo imesaidia kutoa Elimu ya Kilimo kwa wakulima wa Pamba ili kuongeza tija ya zao la Pamba.


"Bodi ya Pamba kupitia wasaidizi wenu, timizeni Wajibu...tunampongeza Rais Samia na Waziri wa kilimo Husein Bashe kwa Usimamizi wa sekta ya Pamba...wakulima wako shambani lakini kuna watu kazi yao ni kutukana na kupotosha jitihada za Serikali" amesema na kuongeza.


"Wapo wanasiasa wanaingilia hapa kati, nitahadharishe katika kipindi hiki, Siasa ikae pembeni tuache utaalamu ufanye kazi...kiongozi yoyote akifabya ubadhirifu wa pembejeo za Pamba atachukuliwa hatua sababu kuiba mbegu za Pamba ni kurudisha nyuma Maendeleo ya wakulima na kuihujumu serikali".


Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wakulima wa Pamba kutochafua Pamba pia viongozi wa vyama vya ushirika (Amcos) kuwa waaminifu kwa kutoa bei halisi pindi inapobadilika.



Awali Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania, Marco Mtunga amesema wakulima wa Pamba hawawezi kupata bei nzuri kama hawazingatii Ubora wa Pamba. 


Ameeleza kuwa katika Msimu ujao, Maafisa Kilimo watasaidia kutengeneza mbolea ya kupulizia ya Maji ili mkulima aweze kutumia mbolea na kupaa tija.



Mwisho.


Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga akiongea wakati wa uzinduzi wa Msimu wa ununuzi wa Pamba.



Mkuu wa Mkoa Simiyu, Kenan Kihongosi akiongea wakati wa uzinduzi wa Msimu wa ununuzi wa Pamba.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI