NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA MWANZA.
Mradi wa ujenzi wa Daraja la JPM linalounganisha Wilaya ya Misungwi na Sengerema Mkoani Mwanza lilogharimu kiasi Cha Bil, 700 umefikia asilimia 99 ili liweze kukamilika .
Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji Mkuu wa Serikali Greyson Msigwa mara baada ya kufanya ziara katika Daraja hilo na kujionea hatua ya ujenzi ulipofikia ambapo kwasasa yamebakia marekebisho madogo ili kukamilika.
Msigwa ameeleza kuwa kukamilika kwa daraja hilo linakwenda kuchochea uchumi kwa kushirikisha Nchi jirani na kutatua changamoto ya usafiri kwa wakazi wa Kanda ya ziwa ambao ulikuwa wanavuka kwa kutumia vivuko kwa zaidi ya masaa nne.
"Kupitia Daraja hili kuna namna ambavyo tunakwenda tunakwenda kuchochea uchumi kwa kushirikisha Nchi jirani pamoja na kuwa kiungo cha usafirishaji kwa Nchi za Burundi, Rwanda, Kongo pamoja na Uganda" Alisema Mabingwa.
Kwa upande mwingine Msingwa amesema kuwa daraja hilo litadumu kwa muda wa miaka mia moja ambapo siku nyingi litaanza kufanya kazi ili kuondoa changamoto ya wananchi kusubiri kivuko kwa muda mrefu
Aidha kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa ujenzi huo Mhandi Wiliam Sanga kutoka Tanroad amesema kuwa tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi huo jumla ya ajira 33505 ambapo wazawa ni asilimia 91.9 ambapo mpaka sasa wamemlipa mkandarasi shilingi Bilioni 539 .
Katika ziara hiyo ya Msemaji mkuu wa serikali ametembelea na kukagua pia mradi wa ujenzi wa vivuko 5 vinavyojengwa na Songoro Marine pamoja ujenzi wa meli ya Mv Mwanza.
0 Comments