Header Ads Widget

SERIKALI YAPANDISHA KIMA CHA CHINI MISHAHARA KWA ASILIMIA 35.1

 


MWANDISHI WETU, MATUKIO DAIMA APP.

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa  Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa mwaka huu Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1% ambapo kwa ongezeko hili sasa kima cha chini kitapanda kutoka 370000 hadi 500000.

Akiongea leo May 01,2025 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mkoani Singida, Rais Samia amesema "Mwezi May mwaka jana wakati wa Siku ya Wafanyakazi Serikali ilieleza ugumu wa uchumi ulivyokuwa wakati ule na kuwasihi tusiongeze gharama kwa Serikali kwa kuongeza mishahara bali tuliendelea na upandishaji wa madaraja na kutoa maslahi mengine ya Wafanyakazi"

"Sasa kwa mapenzi makubwa na kwa namna mlivyoiunga mkono Serikali ilipowaomba mfunge mkanda na mkaamua kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kufanya uchumi wetu ukue kwa 5% mwaka huu, kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Wafanyakazi oyeee, miamvuli oyee, naona miamvuli imepanda sasa wakati wote ilikuwa chini sasa imepanda"

"Sasa kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Mimi na wenzangu na baada ya kuangalia uchumi ulivyopanda na umepanda kwasababu ya nguvu zenu Wafanyakazi, ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1%, Wafanyakazi oyeee"

"Nyongeza hii itakayoanza kutumika mwezi July mwaka huu itaongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 370000 hadi Tsh. 500000, ngazi nyingine za mshahara nazo zitapanda kwa kiwango kizuri jinsi bajeti inavyoruhusu lakini nataka niwaambie nyongeza nzuri ipo"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI