Header Ads Widget

"NANI ANAEWEZA KUTIKISA MEZA YA VIVYWAJI VYA GHARAMA KIZEMBE NAMNA HII"

 

Anaandika Gibson G Bayona

Nimebahatika kwa kipindi cha miaka ya nyuma kidogo kujikita katika maswala ya uchambuzi hususani wa siasa za nchi yetu, leo nimewiwa kurejea tena kwenye tasnia hiyo; ninaanza kwa kuungana na watanzania wengine kuonesha masikitiko ya tukio la kushambuliwa kwa Katibu wa TEC Father Kitima na kulaani vikali na kusisitiza wahusika kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

Baada ya tafakuri nzito na uzoefu wa mambo machache ambayo nina uelewa nayo naweza kusema wazi kuwa Nitakua wa mwisho kuamini hiki kinachoendelea leo ya kwamba kwanamna moja ama nyingine Serikali inaweza kuhusika na tukio la Father Kitima.

Mimi nimeamua kujifikirisha bila mhemko, kwa utulivu tu na ujuzi wangu mdogo kuna kitu kinaitwa Conspiracy theory, sitoeleza undani wake sasa lakini katika fikra za kawaida kwanini kwa haraka haraka tunaweza kuhitimisha kirahisi rahisi tu na kwa jazba sana kwamba serikali hii inaweza kuwa haina mikakati ya kisiasa na kujua impact ya jambo mahususi hadi ifanye kosa kama hili la wazi ambalo ni bayana kuna dhana ya Predictability ya kwamba ni wazi lawama zote na vidole vitanyooshwa kwake?

Kipindi tulichopo sasa ni kipindi cha kipekee sana na mtego mkubwa kwa nchi yetu, Tunapoelekea Uchaguzi Mkuu, kuna mengi yanakuja na ninaamini yatatutikisa sana kama Taifa hususani mikakati miovu ya kuichafua Serikali na kuitengenezea chuki dhidi ya wananchi na target ikiwa ni moja kwa moja Kwa Mhe Rais wetu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambae amejipambanua vyema na watanzania kuendelea kumuunga mkono akiongozwa na subira na ustahimilivu lakini akiwa makini na ulinzi wa Amani na utulivu wa nchi yetu.

Ninatahadharisha kuwa Itakuja mikakati mingi sana ya maksudi na isiotabirika kama huu ambao mimi nimechagua kuwa wa mwisho kuamini ni mkakati wa mfumo nikiamini bali ni mkakati wa wanaotaka kuamsha hasira za Viongozi wa Dini,na hata makundi mengine yenye ushawishi katika jamii ili kuleta taharuki. 

Ni mtego mkali sana huu kwani waliofanya hili wamepiga hesabu zao vizuri sana,(political calculations), wamepanga vema upepo wa kisiasa na wame target mhusika ambae ni rahisi sana kuleta taharuki kwa haraka na ku catch attention ya watu. 

Mungu Ibariki 🇹🇿

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI