Header Ads Widget

SERIKALI IMEFUTA KODI YA VAT KWA NYUMBA ZENYE CHINI THAMANI YA SHILINGI MILIONI 50

 


NaPamela Mollel Arusha

 

Serikali imewataka wamiliki wa nyumba pamoja na wadau wa ardhi[Real Estate) kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwekeza zaidi kwenye ardhi kwa kuwa tayari serikali  imefuta kodi ya ongezeko la thamani VAT kwa nyumba zote zenye thamani ya shilingi Milioni 50 ilinkuboresha maendeleo ya makazi


Hayo yameelezwa na Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Deogratius Ndejembi wakati akifungua mkutano Mkuu na kongamano la tano Chama wataalamu wa miliki kuu Tanzania (AREPTA)jijini Arusha 



Waziri huyo alisema kuwa awamu ya sita imeamua kuboresha mazingira ya ardhi,kwa wawekezaji ili waweze kufungua mazingira hasa ya utalii


"Utalii unapokuwa ardhi nayo inatakiwa sasa nitoe wito kwa wamiliki wa ardhi kuhakiisha kuwa wanawekeza zaidi kwa kuwa serikali imeweka mazingira mazuri na ya kuaminika"aliongeza Waziri huyo 



Katika hatua nyingine alisema kuwa serikali inatarajia kuzindua mpango maalumu wa sheria wa Real Estate ambapo mpango huo utaweza kufungua fursa zaidi 


"Kwa muda huu nyumba ambazo thamani yake haizidi kiasi cha Milioni 50 hazitatozwa kodi ya ongezeko la thamani[V AT] hii ni fursa kwa wawekezaji hasa wazawa kuichangamkia ili kila mtu aweze kumiliki ardhi pamoja na nyumba"alisema waziri



Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wataalam wa Miliki Tanzania (AREPTA)Andrew Kato anasema kuwa  mkutano huo umewakutanisha wataalamu kutoka ardhi,wathamini na wataalamu wanaofanya uchambuzi yakinifu wa miradi ya Miliki


Ameongeza kuwa wanashirikiana na Jumuiya ya wataalamu wa miliki Afrika ambapo wanaongozwa na kaulimbiu inayosema "Uboreshaji wa miundombinu ya usafiri katika miliki kuongeza thamani ya ardhi Afrika Mashariki

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI