Header Ads Widget

NHC YAWASIHI WAPANGAJI JENGO LA LOTTO KUONDOKA.

Na Lilian Kasenene,Morogoro Matukio DaimaApp 

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa wa Morogoro limewasihi wapangaji wanaotumia jengo wanalomiliki kwa ubia na mwekezaji wa Sameer Ismail maarufu kama Lotto kuondoka kwa hiyari ili kipisha matengenezo wanayotatajia kufanya baada ya mwekezaji huyo kutumia muda mrefu kukamilisha ujenzi.

Meneja wa NHC mkoa wa Morogoro Lwitiko Ndigha alisema hayo baada ya Waandishi wa habari kufika ofisini kwake ili kupata majibu ya sintofahamu yaliyotajwa na baadhi ya wapangaji kwenye jengo hilo ambao hawakutaka majina yao kuandikwa kwa madai shirika hilo limewapa notisibya siku Saba kuondoka.

Ndigha alieleza kuwa ni kweli wana ubia na mwekezaji huyo Lottos na wamefanya nae vikao mbalimbali ambavyo walimwagiza kwamba awaondoe wapangaji ili Shirika liweze kumaliza kwa ubora.

"Kwa kuwa alikuwa akilijenga kwa miaka mingi na hajalimaliza muda mrefu tunataka kulimalizia na tumemwagiza awatoe hao wapangaji,"alisema.

Aidha alisema baada ya kushindwa kufanya hivyo Shirika limewapa notisi hao wapangaji kwa kuwataka watoke na kwamba kuna wachache wamepokea na wachache hawajapokea, waliopokea ndo wamepawe notisi waweze kuondoka na ndio watapewa kipaumbele Cha kupanga jengo hilo mara baada ya kumaliza ujenzi

Baada ya kuzungumza na meneja wa NHC, mwandishi wa Habari hii alimtafuta mwekezaji wa jengo hilo Sameer Ismail(Lottos)kuzungumzia sintofahamu hiyo ambaye alisema kuwa kuna hatua tayari amechukua hadi katika umaliziaji wa ujenzi wa jengo na lilipofikia Sasa.

Alisema Mwaka 2006/2007 aliingia mkataba na Shirika la Nyumba na kuanza ujenzi, ambapo walimtaka ajenge jengo la gorofa sita lakini yeye aliwaeleza kuwa ana uwezo wa kujenga jengo la gorofa tatu,ambapo aliwatoa hofu wapangaji na wananchi kuwa jengo liko Salama kwa sababu amefuata vigezo vyote.

Alipoulizwa juu ya wapangaji kupewa notisi na NHC, Lottos aliktaa kuzungumzia suala hilo la notisi kwa wapangaji kwa madai kuwa suala hilo lipo mahakamani kwa Sasa.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI