Header Ads Widget

PSPTB YAWAASA WANAFUNZI 'UOI' KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA USAWA BILA UPENDELEO.

 Berdina Majinge, Matukio Daima.

Wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi katika Chuo kikuu cha Iringa wameashwa kuipenda taaluma hiyo,kwani kupenda wanachokifanya watakifanya kwa weredi na sio kufanya kwa sababu inawabidi wafanye.

Rai hiyo imetolewa na Afisa masoko kutoka bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi Tanzania (PSPTB) Dickson Mollel wakati akitoa elimu kwa wanafunzi  namna bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi inavyofanya kazi.

Mollel alisema kuwa  matokeo ya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ni kwamba wataiokoa nchi au taasisi husika katika janga la hasara kwa sababu fedha nyingi za serikali zinatumika kufanya manunuzi ya huduma au vifaa.

"Tunaendelea kutoa rai kama bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi kuzingatia maadili na kuacha tamaa ya kutaka kumiliki vitu vikubwa vingi kwa muda mfupi kwani kila mtu atafanikiwa kwa wakati kwa jinsi anavyo jituma kufanya kazi kwa weredi kwa kufuata maadili na taratibu ambazo zimewekwa"

"Kufanyakazi unayoipenda kwa moyo kutakufanya kuzingatia maadili, uwazi na usawa bila upendeleo kwa sababu kwa sasa serikali imeweka mifumo ya kidigitali katika uombaji wa tenda za serikali"alisema Mollel

Aidha Mollel aliongeza kuwa kuna baadhi ya watu wanaofanya shughuli za manunuzi bila kufuata maadili wengi wao wanaingiza taasisi hizo kwenye hasara huku ni baadae kwa ukubwa wake nchi ndio inaingia kwenye hasara.

Mollel aliwataka wanafunzi wa fani hiyo kujisajili na kutambulika na bodi  kwa ajili ya ukuaji kwenye taaluma yao ili waweze kufanya na mitihani ya bodi.

"faida ya Mwanafunzi kujisajili ni kutambulika na bodi,ili aanze kupata faida kuanzia akiwa chuo lakini pia akitoka nje zitamsaidia kwa sababu watu ni wale wale ambao amnapaswa kuwa nao kwa ajili ya kupata ajira"



"Natamani kila mwanafunzi aone umuhimu wa kuwa katika shirikisho mapema, baada ya muda watatoka katika mazingira ya shule na kwenda mtaani ambapo watateseka kuitafuta netweki ambayo waliicha humu ndani"

Alisema kuwa Bodi mbali na kusimamia maadili yao katika kutekeleza majukumu yao bodi ikiwafahamu itawalinda wale wanaofanya kila kitu kuhusu manunuzi na ugavi chini ya mwamvuli wa bodi.

"Bodi kazi yake sio kuwaadhibu pale wanapokosea bali hata kuzungumza kwa niaba yao pale inapotokea kwa sababu wanawafahamu"alisema

Kwa upande wake Afisa Ununuzi PSPTB Gabriel Mwakipesile alisema kuwa bodi inahitaji watu wenye maadili wakati wote kwa sababu kazi hiyo inavishawishi vingi.

Mwakipesile alisema kuwa lazima watambulike na bodi na bodi hiyo iweze kufuatilia nyendo zao kimaadili.

"Mtu haruhusiwi kufanya kazi za ununuzi na ugavi kama utambuliki na bodi pia huwezi kupata kazi bila kusajiliwa na bodi kwa hiyo mnapaswa kujisajili kwenye mitihani na kwenye mfumo"alisema Mwakipesile.

Naye Gladness Kawanga mwanafunzi wa manunuzi na Ugavi katika Chuo Kikuu cha Iringa alisema kuwa yupo tayari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na vigezo vilivyowekwa na bodi.

"Mimi niko tayari kujisajili na kufanya kazi kwa uadilifu bila upendeleo kwa sababu fani hii naipenda kutoka moyoni na ninaamini nikihitimu nitafuata utaratibu wa usajili ili nitambulike na bodi"

Mwanafunzi Haile Nsekela alisema kuwa yupo chuoni hapo kusomea fani hiyo kwa sababu anajiamini katika utendaji kazi wake.

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI