Na. Mwandishi Wetu, Dar
NAIBU Katibu Mwenezi Ngome ya Wanawake Chama Cha ACT- Wazalendo ambaye pia ni Mwenezi Jimbo la Kawe, Bi. Glory Tausi Shayo amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Kawe, katika uchaguzi Mkuu Oktoba 29,mwaka huu.
Glory Tausi amekabidhiwa fomu hizo za kugombea Ubunge Kawe, mapema leo Agosti 24, 2025 kwa Msimamizi wa Uchaguzi, Bi. Magreth Mangasa, katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni.
Aidha, Glory Tausi amesema kuwa amepokea fomu hizo baada ya kuteuliwa na Chama chake cha ACT-Wazalendo, kuwa mgombea katika Jimbo hilo la Kawe.
"Tukio hili lenye furaha lilishuhudiwa na maofisa wa Halmashauri. Ninaimani kwa ushirikiano wa wadau wote, tutaibuka na ushindi na kuipatia Kawe uwakilishi bora.
Nguvu Yetu ni Kawe Yetu. KAWE MPYA: Maji, Barabara, Ajira na Afya Bora kwa Kila Mwana Kawe." Amesema Glory Tausi.
![]() |
Glory Tausi akiwa na fomu za kugombea Ubunge Jimbo la Kawe |
0 Comments