Na Lilian Kasenene,Morogoro
Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA kimeendelea kuimarisha ushirikiano na nchi za Nordic kwenye nyannja mbalimbali ikiwemo ya kubadilisha Walimu na wanafunzi.
Makamu mkuu wa Chuo hicho Cha SUA Prof.Raphael Chibunda alieleza hayo mara baada ya mabalozi wa nchi za Sweden, Norway, Denmark, na Finland kutembelea chuoni hapo na kufanya majadiliano juu ya ushirikiano walionao wa muda mrefu.
Prof. Chibunda alisema serikali na wananchi wa nchi hizo wamekuwa na ushirikiano wa muda mrefu ambapo alitolea mfano wa nchi ya Norway ambayo ilikuwa ya kwanza kuhamasisha taaluma ya degree ya misitu na imeendeleza kusaidia katika mambo mengine mbalimbali na nchi ya Denmark ilikuwabya kwanza katika kusaidia ujenzi wa jengo la ndaki ya tiba ya wanyama katika Chuo hicho.
"Tumewashukuru na Sasa tumeendelea kusimama kwa nguvu zetu wenyewe na Walimu wetu wenyewe na kumeweza kukipanua chuo kwa sababu ukiangalia wakati wanasaidia kilikuwa na idadi ndogo ya wanafunzi wasiozidi 2,000 ukilinganisha na Sasa ambapo wapo wanafunzi zaidi ya 18,000,"alisema.
Alisema ujio wa nchi hizo walikuja kuona wanaendelezaje na na kwamba utaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano zaidi pamoja na kubadilishana wanafunzi na Walimu wabobezi,wandamizi ili wanafunzi waweze kupata uzoefu zaidi.
Aidha makamu mkuu huyo alieleza kuwa nchi ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo la NORAD Wana mpango wa kutangaza nafasi na kuweka fedha za utafiti hivyo kama Chuo kupitia watafiti wake watahakikisha wanawahamasisha kuchangamkia fursa hiyo na kuwaandaa na ni imani yake kuwa kwa weledi na uzoefu walionao wanaweza kupata baadhi ya miradi.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania Jesper Kammersgaard alisema amefurahishwa kutembelea SUA pamoja na mabalozi wenzake, vyuo vya nchi hizo wataendeleza mashirikiano zaidi.
"Mashirikiano haya kwa nchi hizi za Nordic na nchi ya Tanzania ni wa zaidi ya miaka na miaka tumefurahi sana Sisi kama mabalozi,"alisema balozi huyo.
Katika hatua nyingine balozi huyo wa Denmark Jesper, akizungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake wakiwa katika Ushirika wa Wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA-(Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative (SUGECO), alipongeza Tanzania kutokana na matokeo chanya waliyobaini kwenye sekta ya Mifugo,kuwajengea Uwezi vijana kujiajiri.
Alisema pamoja na eneo la misitu waliahidi ushirikiano zaidi ambao utaelekea kwenye maeneo ya nidhati jadidifu,tafiti,Kilimo na Maendeleo ya jamii.
Mkurugenzi wa SUGECO Revocatus Kimario alisema kazi wanazofanya kwa ushirikiano na nchi za Denmark,Norway, Sweden na Finland ni kuona mikakati wanazofanya na moja wapo ni kuwapeleka vijana kwenye nchi husika ambapo mpaka sasa vijana 850 kwa miaka miwili wamepelekwa, 2023-vijana 535 walipelekwa na wanaendelea kupelekwa.
Pia alisema kwa sasa wako kwenye mikakati wa kuanzisha kituo Cha umahili Cha uzalishaji wa mbegu za nguruwe kwa Morogoro kwa kushirikiana na kampuni za Denmark.
Ziara hiyo ya mabalozi mkoani Morogoro wametembelea pia kituo Cha kuzalisha mbegu za miti kilichopo chini ya Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) ambapo walishiriki upandaji miti.
0 Comments