Header Ads Widget

MTENDAJI KATA MBARONI TUHUMA ZA RUSHWA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Afisa Mtendaji wa Kata ya Rungwe Mpya halmashauri ya wilaya Kasulu Tausi Issa Manyanya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma akikabiliwa na tuhuma za  kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Manyanya alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo ya wilaya na kusomewa Shauri hilo la jinai namba CC 11711/2025  mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo. Emaculate Shulli ambapo Mtuhumiwa  anakabiliwa na makosa mawili chini ya kifungu cha 15(1)(a) na 15(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022.

Waendesha Mashtaka wa Serikali kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) James Mosi Nyarobi na Bw. Davis Jason Junior Katika  hati ya mashtaka walieleza kuwa Mtendaji huyo anadaiwa kuwa akiwa katika kijiji cha Rungwe Mpya wilaya ya Kasulu alidai na kupokea hongo ya shilingi 210,000 kutoka kwa mfugaji aliyetambulika kwa jina la Omari Haruna  mkazi wa Kijiji cha Kigembe wilaya ya Kasulu.

Katika hati hiyo ya Mashitaka Mtenda huyo anadaiwa kupokea fedha hizo ili kuruhusu kurudishwa kwa ng’ombe mmoja wa mfugaji ambaye aliyepotea na kupatikana katika kijiji hicho Kigembe aliyekutwa amehifadhiwa  kwa mfugaji,  Longo Lugata Shija kwa maelekezo ya Afisa Mtendaji huyo wa kata.

Mtendaji huyo wa Kata ya Rungwe Mpya  alikana mashtaka yote mawili yaliyosomwa mbele ya Mahakama hiyo ambapo Mahakama ilimpa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa, na shauri hilo limepangwa  kusikilizwa tena tarehe 02,  Juni mwaka huu.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI