Na Matukio Daima App.
LUSHOTO.Mkuu wa wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye amekabidhi refrector 1000 kwa vijana wa bodaboda ambapo 200 kati yao wamejiandikisha kwa kupiga kura ikiwa ni hamasa kwa uandikishaji wa wapiga kura awamu ya pili wilayani Lushoto mkoani Tanga.
Hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Nyerere square wilayani Lushoto wakati Mkuu wa wilaya Sumaye akihamashisha Vijana kushiriki kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Amesema lengo kuu la kuwakabidhi vijana hao reflector hizo ni kutoa hamasa kwa vijana ili washiriki katika uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge pamoja na Madiwani mwezi Oktoba mwaka huu 2025.
Hata hivo katika mkutano huo wa ugawaji wa refrector hizo vijana zaidi ya 200 wa bodaboda ambao hawajajiandikisha na kusema kua wako tayari kujiandikisha kutokana na hamasa kubwa walioipata kutoka kwa Mkuu huyo wa wilaya.
Amesema refrector hizo ni uniform zao za kuwatambua vijana hao katika vijiwe vyao na kuwasisitiza kuwa kila dereva wa bodaboda lazima awe na namba yake kwaajili ya utambuzi ili hata ikitokea tatizo watambuane kwa urahisi.
MWISHO.
0 Comments