Na Matukio Daima Media
SHULE ya Sekondari St Anne Marie Academy imekuwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwa mara nyingine tena kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka huu kwa kufaulisha wanafunzi wengi kwa daraja la kwanza na la pili.
Kwenye matokeo hayo yaliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani NECTA jana, wanafunzi 51 wa shule hiyo iliyoko Mbezi Kimara kwa Msuguli walipata daraja la kwanza, wanafunzi 84 daraja la pili na wanafunzi 74 daraja la tatu.
Mkuu wa shule hiyo Edrick Phillemon alielezea kufurahishwa na matokeo hayo akisema kuwa shule hiyo imekuwa ikipokea wanafunzi wenye wastani wa kawaida na kuhakikisha wanawafundisha hadi kupata daraja la kwanza na la pili na wachache sana daraja la tatu.
Alisema tofauti na shule zingine zinazochukua wanafunzi wenye ufaulu mkubwa, St Anne Marie imekuwa ikichukua wanafunzi wa kawaida bila kubagua hata wenye wastani mdogo kwa kuwa inajiamini kuwa na walimu mahiri wenye uwezo wa kuwaandaa kwaajili ya mitihani ya mwisho na wakafanya vizuri.
“Kwetu haya ni matokeo mazuri sana ukizingatia sisi hatubagui wanafunzi tunachukua wenye wastani wa kawaida sana kwasababu tunawaamini walimu wetu ambao wanafanyakazi usiku na mchana, mwanafunzi akija kwetu hata awe na wastani mdogo kwenye mtihani wake wa mwisho atafanya vizuri kwasababu ya umahiri wa walimu wetu na miundombinu mizuri ya shule,” alisema
“Kipekee nampongeza Mkurugenzi wa shule ya St Anne Marie Academy Dk Jasson Rweikiza kwa kuiwezesha shule hii kuwa na miundombinu ya kisasa kama maktaba zenye viyoyozi, maabara, madarasa na walimu mahiri wa masomo yote na haya kwa ujumla ndiyo siri ya mafanikio ya shule hizi,’ alisema
“Hata lishe ya wanafunzi hapa St Anne Marie Academy ni ya kipekee wanafunzi wanakula hadi milo minne kwa siku tuna bustani za mboga mboga matunda, Mkurugenzi ameweka utaratibu wa motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri kwenda kwenye mbuga za wanyama kama Setengeti, Ngorongoro na Mikumi na kupewa fedha taslim motisha kama hii ni miongoni kwa vichocheo vya sisi kupata matokeo mazuri,” alisema
Alisema Mkurugenzi wa shule hiyo amekuwa msaada mkubwa kwa kuweka bodi ya mitihani shuleni hapo ambayo kazi yake ni kutunga mitihani na kufuatilia maendeleo ya taaluma ya wanafunzi wa shule hiyo.
Hivi karibuni Mkurugenzi na Mwanzilishi wa shule hiyo, Dk Jasson Rweikiza, alisema shule hiyo iliamua kuweka bodi ya mitihani shuleni hapo ili kuongeza ubora wa taaluma.
“Mwalimu hapa St Anne kazi yake ni kufundisha kazi ya kutunga mitihani imepewa bodi ya mitihani kwasababu tuliona mwalimu akifunsisha mwenyewe akatunga mitihani mwenyewe anaweza kupendelea kwenye silabasi alizofundisha tu akaacha zile ambazo hakuzikamilisha,” alisema
“Sasa bodi ikitunga mitihani kama silabasi zilikuwa tano watatunga mtihani kwenye silabasi zote na mwanafunzi akifeli mwalimu atapaswa kujieleza kwanini wanafunzi wamefeli mtihani wake,” alisema Dk. Rweikiza
Mwisho
0 Comments