Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
WAKULIMA wa Mpunga wa kijiji cha Mandaka Mnono katika Kata ya Oldmoshi Magharibi mbioni kunufaika na mradi mkubwa wa umwagiliaji ambao unajengwa na serikali kwa gharama ya Shilingi bilioni 5.1.
Hatua hiyo inatoa pongezi nyingi kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huu.
Mradi huo mkombozi unakwenda kuwawezesha wakulima walime kwa uhakika kwa misimu yote na kwa kuvuna mara tatu kwa mwaka.
Mradi huu unalenga kusaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza utegemezi wa mvua na baadaye kujiongezea kipato na kulikwamua taifa na baa la njaa.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi na Diwani wa Kata, Peter Massawe wamechangia kwa kiasi kikubwa kwenye utekelezaji wa mradi huu.
Mwisho..
0 Comments