Na Shomari Binda-Matukio Daima
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) TaifaJoyce Mang'o, amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa msaada wake wa kisheria kwa watanzania.
Shukrani hizo amezitoa jana mei 10,2025 visiwani Zanzibar aliposhiriki tukio la uzinduzi wa kampeni ya Mama Samia Legal Aid ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Dkt.Hussen Ally Mwinyi.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo amesema kampeni hiyo imekuwa msaada mkubwa tangu ilipozinduliwa nchi nzima.
Amesema amepita maeneo mengi na kusikia sauti za wanufaika wa msaada huo wa kisheria hasa wanawake wakimshukuru Rais Dkt.Samia.
Mnec huyo amesema wapo wanawake waliotatuliwa matatizo yao papo kwa papo na wale wenye kesi Mahakamani wamepatiwa mawakili wa kuweza kuwasaidia.
" Tunamshukuru sana mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na kuanzisha kampeni hii ya msaada wa kisheria." Amesema na kuongeza.
" Kila nilipohudhuria uzinduzi wa kampeni nimeona namna watanzania wavyotoa shukrani zao kwa namna walivyosaidiwa kwa kupata msaada huu",amesema.
Mang'o amesema namna ya kumlipa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni watanzannia kumchagua kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.
Baadhi ya wanufaika wa msaada huo wa kisheria waliozungumza na Matukio Daima wamesema kumpata mwanasheria wa kusimamia kesi ni gharama lakini kupitia kampeni hiyo imekuwa mkombozi.
Mwisho.
0 Comments