Na Mwandishi wetu, Busega.
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mkoani Simiyu wametakiwa kushirikiana na watendaji wa serikali katika usimamizi wa zao la pamba ili kuwezesha halmashauri kupata mapato yatakayowezesha kumpeleka huduma kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Faidha Salimu ametoa wito huo, wakati akitoa salam za serikali katika kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, huku akiyaonya makampuni yatakayojaribu kutorosha pamba.
Amesisitiza lazima wanunuzi wa pamba wanunue na kusafirisha pamba kwa kuzingatia miongozo ya serikali, na kwamba atakayeenda kinyume atachukuliwa hatua.
Tayari Makampuni 14 yamepitishwa kununua zao la pamba wilayani Busega katika msimu wa mwaka 2025/2026.
Mwisho.
0 Comments