Header Ads Widget

MLIPUKO KATIKA BASI LA SHULE NCHINI PAKISTAN WAUA TAKRIBANI WATU WATANO

 

Mlipuko wa basi la shule katika eneo la Balochistan nchini Pakistani umesababisha vifo vya takriban watu watano na kujeruhi makumi.

Basi hilo lilikuwa limebeba watoto wa shule 40 wakati lilipolipuka mwendo wa saa 07:40 saa za huko (02:40 GMT) nje kidogo ya mji wa mbali wa Khuzdar, polisi waliambia BBC.

Watu watatu kati ya watano waliouawa ni watoto, polisi walisema.

Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha mabaki ya basi kubwa lililoteketea, huku mikoba ikiwa imetapakaa pembeni yake.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na tukio hilo hadi sasa, lakini Balochistan, jimbo lenye machafuko kusini magharibi mwa nchi hiyo, limekuwa likikumbwa na uasi wa muda mrefu na ukiukaji wa haki za binadamu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI