Na Fatma Ally Matukio DaimaApp, Dar
KATIBU Mkuu Wizara ya Mali Asili na Utalii Dkt Hassan Abbas amesema wamekuwa na mashirikiano mazuri na nchi ya Finland hasa katika maeneo ya misitu na kubadilishana wataalam .
Hayo ameyaeleza leo jijini Dar es Salaam wakati mke wa rais wa Finland alipotembelea makumbusho ya taifa ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo pamoja na utamaduni wa mali kale.
Dkt Abbas amesema licha ya fast lady huyo kitembelea makumbusho hiyo Pia mume wake nae kesho atakwenda kutembelea makumbusho hayo ambe ni Rais wa finland.
Katika ziara hiyo fupi ya Rais wa finland kwenda kutembelea nchi ya Tanzania pia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hivi karibuni atazindua mradi wa dola Pound mill 20 sawa shi mill 40 za Kitanzania ambao ni mradi mpya utakaosaidia kukuza na kuendeleza sekta ya misitu.
"Nchi yetu imekua na mashirikiano makubwa na nchi ya Finland kwani sisi ni marafiki wa muda mrefu ambapo hata Rais Hayyat Mwl Julius Nyerere miongoni mwa ziara zake za mwaka 1973 alitembelea nchini Finland"
Amesema kuwa, ukienda Finland nchi yake ni ya misitu, uchumi wake kwa kiwango kikubwa unategemea misitu hata ukienda kutembelea vituo vyao kwa kiwango kikubwa unaona uhalisia wanategemea misitu na hata Taasisi zao tafiti zao nyingi zinaegemea kwenye eneo hilo.
"Sisi wizara ya mali asili na utalii tunanufaika sana na wenzetu wa Finland hasa katika sekta ya misitu, tuna ushirikiano wa zaidi ya miaka 40, miradi ambayo tumekuwa tukiifanya inayohusu misitu na mazao yake, huu mradi ambao tutausaini kesho kutwa ni muendelezo wa haya yote ambayo wamekuwa wakitusidia"
Aidha amesema kuwa, Finland wanatarajia kuekeza uro mill 20 kwenye mradi mpya ni kitu kikubwa kwa nchi ya Tanzania ambapo kwenye sekta ya misitu wameendelea sana, wanatumia misitu kama chanzo cha bidhaa za viwandani pia wamewasaidia kuonyesha wamewekeza utalii kwenye misitu .
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema ujio wa mke wa rais kutoka Finland ni mafanikio makubwa ya Serikali ya awamu ya sita katika kuutangaza utalii lakini pia ni alama kwa Wizara ya mali asili na utalii katika kupanua wigo wa kutangaza vivutio vya utalii.
"Tulizoea wageni kwenda kutalii mbuga za wanyama lakini sasa wanakuja kwenye makumbusho, ni uwekezaji mkubwa ambao Wizara ya mali asili na utalii imefanya katika kufungua mazao ya utalii, pia ni wananchi wa Tanzania na wageni watembelee makumbusho zetu kwani ukifika taifa lolote ukitaka kujua historia yao ni lazima utembelee mali kale hasa makumbusho ya taifa"amesema Dkt Lwoga.
Ameongeza" Hii sasa ni hamasa kwa watanzania na wageni waendelee kutembelea makumbusho ya taifa kwa ajili ya kujifunza historia ya taifa, utamaduni na urithi, kufahamu muingiliano wa nchi hii na mataifa mengine na mashirikiano mazuri baina ya nchi na mataifa mengine..."
Aidha, amesema makumbusho ya taifa wanashughulika na tafiti ukusanyaji, uendelezaji na kutoa elimu kwa Jamii, hivyo wangependa kushirikiana na nchi ya Finland katika katika kufanya utafifi katika eneo la tamaduni na mali kale kwani wao wamepiga hatua katika eneo hilo.
Ameeleza kuwa eneo jengine ni uhifadhi na makusanyo ya kihistoria kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi hivyo wakishirikiana nao wanaweza kupata miundombinu mizuri ya kitenlojia na uwelewa wa uhifadhi wa mali kale na utamaduni kwa njia ya kisasa .
Hata hivyo, amesema ujio wa Rais wa Finland kesho pia kutembelea makumbusho ya taifa si tu kuacha alama mashirikiano mazuri yaliopo baina ya nchi hizo mbili bali kuwakumbusha watanzania kupenda na kuthamini vitu vya kwao.
"Kumekua na mashirikiano mazuri baina ya Finland na Tanzania, ujio wao nchi inakwenda kuimarisha mahusiano hayo pia eneo la makumbusho litaendelea kufunguka kwa wageni wanapofika nchi kuja kutembelea makumbusho zetu na kujifunza historia na tamaduni za malikale"
0 Comments