Header Ads Widget

HECHE AWAOMBA WANANCHI MUSOMA KUIUNGA MKONO CHADEMA"NO REFORMS NO ELECTION"

 

Na Shomari Binda,Matukio Daima Media ,Musoma 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) John Heche amewaomba wananchi na wanachama wa chama hicho kuunga mkono kampeni ya " No Reforms No Election inayoendelea nchi nzima.

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika leo mei 14,2025 kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo amesema kuna maana kubwa ya kile wanachotaka kifanyike kabla ya kuingia kwenye uchaguzi.

Amesema kuingia kwenye uchaguzi bila kuwa na mabadiliko ya taratibu za uchaguzi hawawezi kushiriki kwa kuwa haina maana.

Heche amesema moja ya jambo ambalo hawakubaliani nalo ni uchaguzi kusimamiwa na mkurugenzi na mtendaji ambao wanateuliwa na Rais.

 Amesema kama utaratibu huo utaendelea hawawezi kuingia kwenye uchaguzi huo na ndio wanaendelea kuzunguka na kuwaeleza wananchi na kuomba kuungwa mkono.

Makamu Mwenyekiti huyo amesema mkoa wa Mara ni mkoa ambao umejaaliwa rasilimali nyingi lakini watu wake ni masikini hivyo ni muhimu kukubali mabadiliko.

" Nawashukuru sana ndugu zangu wa Musoma.kwani licha ya mvua kubwa lakini mmedimama na kuweza kutusikiliza kutokana na ujumbe tuliowaletea.

" Naomba murndelee kutuunga mkono na ujumbe wa " No Reforms No Election" maana kuna sababu muhimu ya kampeni hii",amesema.


Aliyekuwa Katibu Mkùu aa chama hicho Wilbrod Slaa amesema mabadiliko ni muhimu kuelekea uchaguzi mkuu na lazima wana Mara wawe srhemu ya mabadiliko hayo.


Amesema wataendelea na kuwafikishia ujumbe watanzania waelewe kile wanachokipigania kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu.


Mkutano huo umehudhuriwa pia na viongozi wengine wa chama hicho ambao kwa nyakati tofauti wameelezea kutokuingia kwenye uchaguzi bila mabadiliko.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI