Header Ads Widget

MHANDISI KUNDO AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KATA ZA MWAUMATONDO NA IHUSI.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, akionyesha moja ya jezi ya kata ya Mwaumatondo ambayo ameikabidhi ili vijana washiriki kwenye michezo.


Na Costantine Mathias, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi  Kundo Mathew amegawa vifaa vya Michezo ikiwemo jezi na mipira kwenye  Kata ya Mwaumatondo na Ihusi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ili kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya michezo.


Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri Maji, amesema anatoa vifaa hivyo ili kutimiza ahadi yake kwa vijana na kuendeleza na kuunga Mkono jitihada za Rais Samia kwenye sekta ya michezo ambapo hata yeye (Mhandisi Kundo) amesema anapenda michezo.



Akiwa kwenye Kata ya Mwaumatondo Leo, May 17, 2025, Mbunge huyo ametoa vifaa vya michezo kwenye Matawi ya Mwabalizi, Mwaumatondo na Mwasinasi ambapo kila tawi limepewa mipira minne na pea moja yenye jezi 16 ambapo zilikababidhiwa kwa viongozi wa kata na Matawi huku pia mipira mitatu na seti moja ya jezi ikitolewa ngazi ya kata Mwaumatondo.


"Vifaa hivi vitawasaidia vijana kujiendeleza kimichezo, michezo itaimarisha Afya na kuibua vipaji kwa vijana watakaoweza kucheza soka la ndani na nje ya nchi...nimetimiza ahadi niliyoitoa kwa vijana" amesema Mhandisi Kundo.


Akiwa katika kata ya Ihusi, Mbunge huyo amekabidhi mipira 19 kwenye Matawi 4 ambapo kila tawi limepatiwa mipira minne na pea moja ya jezi wakati huo kata ikipewa mipira mitatu na jezi pea moja.


Wanufaika wa michezo akiwemo Pande chambani, ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Mwaumatondo, amesema  wanamshukuru Mbunge wao kupatia jezi na mpira ambapo michezo itawajenga kiafya.


Nghabi maige, Katibu UVCCM tawi la Mwaumatondo, anasema "tunamshukuru Mbunge wa Jimbo la abariadi kutupatia jezi na mpira ili kuboresha sekta ya mchezo, kutokana na uhaba wa vifaa vya michezo tuliomba na tumepata, tunashukuru. Tutatuzidi kumuunga mkono Mbunge Kundo."


Fadhili maduhu, anasema wanamshukuru Kundo kuwapa vifaa vya michezo ili kuibua vipaji vipya Kwa vijana huku akimpongeza Mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake kwa vijana.


Kazi Saguda, Katibu UVCCM kata mwaumatondo, vifaa hivyo vya michezo vitasaidia kuibua vipaji vya vijana ambao wataweza kuonyesha uwezo wao.


Mwisho.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, akionyesha moja ya jezi ya kata ya Mwaumatondo ambayo ameikabidhi ili vijana washiriki kwenye michezo.



MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, akionyesha moja ya mpira ambayo ameikabidhi ili vijana washiriki kwenye michezo kwenye Kata za Ihusi na Mwaumatondo.






 
























Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI