NA WILLIUM PAUL, VUNJO.
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Charles Stephen Kimei, ameendelea kuonesha moyo wa uwajibikaji na kujali ustawi wa wananchi wake kwa kuwawezesha wajasiriamali wanawake 300 wa Kata ya Njiapanda, Mji Mdogo wa Himo, kwa kuwapatia miavuli maalum itakayowalinda dhidi ya mvua na jua.
Hatua hiyo imelenga kuwawezesha kufanya shughuli zao za kila siku kwa utulivu na ufanisi zaidi ambapo zoezi hilo litawanufaisha wajasiriamali 2000 Jimboni humo.
Katika tukio hilo lililojawa na hisia, wajasiriamali hao walionesha upendo na shukrani kwa Mbunge wao kwa kumchangia kiasi cha shilingi 260,000 ikiwa ni mchango wa hiari kwa ajili ya kumuwezesha kuchukua fomu ya kuomba uteuzi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) atapojitokeza tena kugombea.
Kitendo hicho ni kielelezo tosha cha imani kubwa waliyonayo kwake kutokana na kazi nzuri anayoendelea kuifanya kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Vunjo.
Mwisho.
0 Comments