Header Ads Widget

SERIKALI KUUNDA TIMU YA WATAALUM WATAKAOSIDIA KUBAINI UDANGANYIFU SEKTA YA BIMA (TIRA)

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MEDIA MWANZA.

Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kuunda timu ya watalaamu watakaowasadia Kubaini udanganyifu unaofanyika na baadhi ya watumiaji wa bima Kwa kusudi la kutaka kujipatia kipato kisicho Cha harali.

Akizungumza na Matukio Daima Meneja wa Kanda ya Ziwa Richard Toyota ameeleza kuwa wamefikia uamuazi huo baada ya watumiaji wa bima kujihusisha na vitendo vya udanganyifu Kwa kunidanganya kampuni ya bima Kwa kutoa taarifa za uongo ili kujipatia fedha.

Toyota amewataka Watumiaji wa bima kuachana na  tabia ya udanganyifu kuwa wamepata majanga wakati sio kweli kwani bima itamlipa mtu fidia kutokana na  majanga yaliyotokea Kwa bahati mbaya au ambayo mhusika hawezi kuyazuia pindi yanapotokea.

"Kama Kuna mtu atakuwa amejitakia majanga mwenyewe Kwa kuviondoa vifaa au Kwa kugonga gari lake mwenyewe makusudi ikithibitika kwamba amejitakia au amesababisha madhara yeye mwenyewe kampuni ya bima haitaweza kumlipa fidia yoyote Ile" Alisema Toyota.

Amefafanua kuwa Serikali imejipanga kuweka mazingira wezeshi Kwa kuweka watu watakaosaidia kufanya uchunguzi wa udanganyifu utakaotokea Kwa watumiaji wa bima kipindi majanga kama hayo yanapotokea na kubainisha kama ubadilifu upo.

"Lazima tutambue kama dunia imebadilika na teknolojia inaongezeka uwezo wa watu kutengeneza matokeo ya uongo ni makubwa zaidi lazima kuwepo na wachunguzi au watalaamu ambao wanaweza kuwa na utalamu zaidi kubaini ubadilifu unaotokea"

Hata hivyo ameeleza kuwa Kuna baadhi ya watu wanaopata changamoto katika biashara zao wanadaiwa mikopo na benki wanaamua kuchoma biashara zao au kutengeneza ajali ya gari Kwa kugonga ili waweze kupata fidia kutoka kwenye makapuni ya bima.

"Ikithibitika umechoma biashara Kwa makusudi ya kutaka kujipatia kipato kisicho Cha harali wewe ni mwalifu kama waalifu wengine hivyo vyombo vya Sheria vitachukua mkondo wake"Alisema Toyota.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI